2 Mambo ya nyakati 15

Asa Afanya Matengenezo

1 Roho waBwanaakamjia Azaria mwana wa Obedi.

2 Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini.Bwanayu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Kama mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini kama mkimwacha yeye, naye atawaacha ninyi.

3 Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria.

4 Lakini katika taabu yao walimrudiaBwana, Mungu wa Israeli na kumtafuta, naye akaonekana kwao.

5 Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa ye yote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa.

6 Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina.

7 Lakini kwa habari yenu ninyi, iweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu.”

8 Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Obedi nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini na kutoka katika miji aliyoiteka ya vilima vya Efraimu. Akakarabati madhabahu yaBwanailiyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu laBwana.

9 Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni waliokuwa wanaishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwambaBwanaMungu wake alikuwa pamoja naye.

10 Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Asa.

11 Wakati huo wakamtoleaBwanadhabihu za ng’ombe 700, kondoo na mbuzi 7,000 kutoka katika zile nyara walizoteka.

12 Wakafanya agano kumtafutaBwana, Mungu wa baba zao kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote.

13 Wale wote ambao hawangemtafutaBwana, Mungu wa Israeli wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke.

14 WakamwapiaBwanakwa sauti kuu, kwa kupiga kelele, tarumbeta na kwa mabaragumu.

15 Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyoBwanaakawastarehesha pande zote.

16 Mfalme Asa akamwondolea Maaka mama yake wadhifa wake asiwe mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza kichakani nguzo ya chukizo ya Ashera. Asa akaikata ile nguzo akaiangusha, akaivunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni.

17 Ingawa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika Israeli, Asa akauweka moyo wake wote kwaBwanakikamilifu siku zote za maisha yake.

18 Akaleta katika Hekalu la Mungu fedha, dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.

19 Hapakuwepo vita tena mpaka mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/15-04520e161cb1855d8372f266d5f43653.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × three =