2 Mambo ya nyakati 23

Uasi Dhidi Ya Athalia

1 Katika mwaka wa saba Yehoyada akaonyesha nguvu zake. Akafanya agano na majemadari wa vikosi vya mamia: Azaria mwana wa Yehoramu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya na Elishafati mwana wa Zikri.

2 Wakazunguka katika Yuda yote na kukusanya Walawi na viongozi wa jamaa za Israeli kutoka katika miji yote. Walipofika Yerusalemu,

3 kusanyiko lote likafanya agano na mfalme kwenye Hekalu la Mungu.

Yehoyada akawaambia, “Mwana wa mfalme atatawala, kamaBwanaalivyoahidi kuhusu wazao wa Daudi.

4 Basi hili ndilo liwapasalo kufanya: Theluthi ya makuhani wenu na Walawi ambao watakuwa kwenye zamu siku ya Sabato watalinda milangoni,

5 theluthi watalinda jumba la kifalme, theluthi nyingine watalinda Lango la Msingi. Watu wengine wote itawapasa wawe ndani ya nyua za Hekalu laBwana.

6 Hakuna ruhusa mtu ye yote kuingia Hekaluni mwaBwanaisipokuwa makuhani na Walawi walioko kwenye zamu. Wao wanaweza kuingia kwa sababu ni watakatifu, lakini watu wengine wote itawapasa kuangalia kile kilichoamriwa naBwana.

7 Walawi watajipanga kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha zake mkononi. Mtu mwingine ye yote aingiaye Hekaluni lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme po pote aendapo.”

8 Walawi na watu wote wa Yuda wakafanya vile vile kama Kuhani Yehoyada alivyoagiza. Kila mmoja akachukua watu wake, wale waliokuwa wakienda kwenye zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakitoka kwenye zamu, kwa sababu Kuhani Yehoyada hakuruhusu kikosi cho chote kiondoke.

9 Kisha akawapa majemadari wa vikosi vya mamia mikuki na ngao kubwa na ndogo zilizokuwa mali ya Mfalme Daudi na ambazo zilikuwa ndani ya Hekalu la Mungu.

10 Akawapanga walinzi kumzunguka mfalme, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi. Wakakaa kwenye mduara kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini wa Hekalu wakiizunguka madhabahu yote.

11 Yehoyada na wanawe wakamtoa nje Yoashi mwana wa mfalme nao wakamvika taji wakampa nakala ya Agano na kumtangaza kuwa mfalme. Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, nao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!”

12 Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akawaendea watu katika Hekalu laBwana.

13 Athalia akaangalia, tazama alikuwepo mfalme akiwa amesimama karibu na nguzo yake kwenye ingilio. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa kando ya mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wanashangilia na kupiga tarumbeta na waimbaji wakiwa na vyombo vya uimbaji, walikuwa wakiongoza nyimbo za sifa. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kupiga kelele, akisema, “Uhaini! Uhaini!”

14 Kuhani Yehoyada akawatoa nje majemadari wa vikosi vya mia, waliokuwa viongozi wa jeshi na kuwaambia: “Mtoeni nje kati ya safu na mkamwue kwa upanga ye yote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Msimwulie ndani ya Hekalu laBwana.”

15 Kwa hiyo wakamkamata alipofika kwenye ingilio la Lango la Farasi katika viwanja vya jumba la kifalme wakamwulia hapo.

16 Kisha Yehoyada akafanya agano kwamba yeye na watu wote pamoja na mfalme watakuwa watu waBwana.

17 Kisha watu wote wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu pamoja na sanamu na kumwua Matani kuhani wa Baali mbele ya hizo madhabahu.

18 Kisha Kuhani Yehoyada akaweka uangalizi wa Hekalu laBwanamikononi mwa makuhani, waliokuwa Walawi, ambao Mfalme Daudi alikuwa amewagawa ili wahudumu hekaluni kwa ajili ya kutoa sadaka za kuteketezwa zaBwanakama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, kwa kushangilia na kuimba kama Daudi alivyokuwa ameagiza.

19 Pia akawaweka mabawabu kwenye malango ya Hekalu laBwanaili kwamba kwa vyo vyote asije akaingia mtu ye yote aliye najisi.

20 Akawachukua majemadari wa mamia, watu waheshimiwa, viongozi wa watu pamoja na watu wote wa nchi na kumteremsha mfalme kutoka hekaluni mwaBwana. Wakaingia kwenye jumba la kifalme kwa kupitia Lango la Juu na kumkalisha mfalme kwenye kiti cha enzi cha ufalme,

21 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/23-b6936cf294b110a947eb1843261e8c10.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × five =