2 Mambo ya nyakati 24

Yoashi Akarabati Hekalu

1 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba.

2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni paBwanamiaka yote ya Yehoyada kuhani.

3 Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike.

4 Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu laBwana.

5 Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.

6 Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada Kuhani Mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Mose mtumishi waBwanapamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”

7 Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwaBwanakwa mabaali.

8 Kwa amri ya mfalme, likatengenezwa kasha, nalo likawekwa nje kwenye lango la Hekalu laBwana.

9 Tangazo likatolewa katika Yuda na Yerusalemu kwamba inapasa wamleteeBwanakodi ile ambayo Mose, mtumishi waBwanaalikuwa amewaagiza Israeli huko jangwani.

10 Maafisa wote na watu wote wakaleta michango yao kwa furaha, wakaweka kwenye kasha mpaka likajaa.

11 Ikawa kila wakati kasha lilipoletwa ndani na Walawi kwa maafisa wa mfalme na kuona kwamba kuna kiasi kikubwa cha fedha, mwandishi wa mfalme na afisa wa Kuhani Mkuu walikuwa wanakuja na kumimina, kisha kulirudisha mahali pake. Walifanya hivi mara kwa mara, nao wakakusanya fedha nyingi sana.

12 Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu laBwana. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu laBwana, pia wafanya kazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu laBwana.

13 Watu walioshughulika na kazi walikuwa wenye bidii, nayo kazi ya kukarabati ikaendelea vizuri mikononi mwao. Wakalitengeneza upya Hekalu laBwanalikarudi katika hali yake ya awali na kuliimarisha.

14 Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu laBwana: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu laBwana.

15 Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku wakati alipokufa. Alikufa akiwa na umri wa miaka 130.

16 Wakamzika pamoja na wafalme katika Mji wa Daudi, kwa sababu ya mema aliyokuwa ametenda katika Israeli kwa ajili ya Mungu na Hekalu lake.

Uovu Wa Yoashi

17 Baada ya kifo cha Yehoyada, wakuu wa Yuda walikuja kumpa mfalme heshima, naye akawasikiliza.

18 Wakaacha Hekalu laBwana, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya kosa lao, hasira ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu.

19 IngawaBwanaaliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.

20 Ndipo Roho waBwanaakaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri zaBwana? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwachaBwana, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”

21 Lakini wakafanya shauri baya juu yake na kwa amri ya mfalme wakampiga kwa mawe mpaka akafa katika ukumbi wa Hekalu laBwana.

22 Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimwua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “Bwanana alione hili na alipize kisasi.”

23 Mwishoni mwa ule mwaka, jeshi la Waaramu likaja dhidi ya Yoashi, likavamia Yuda na Yerusalemu na kuwaua viongozi wote wa watu. Wakapeleka nyara zao zote kwa mfalme wao huko Dameski.

24 Ingawa jeshi la Waaramu lilikuwa limekuja na watu wachache tu,Bwanaakatia mikononi mwao jeshi kubwa kuliko lao. Kwa sababu Yuda walikuwa wamemwachaBwana, Mungu wa baba zao, hukumu ilitekelezwa juu ya Yoashi.

25 Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemwua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamwulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

26 Wale waliofanya hila mbaya dhidi yake walikuwa Zabadi, mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, Yehozabadi, mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabi.

27 Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/24-a1cf888b463e80b8736a814ed1081f27.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × four =