2 Mambo ya nyakati 36

Mfalme Yehoahazi Wa Yuda

1 Watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia na kumfanya aingie mahali pa baba yake kuwa mfalme katika Yerusalemu.

2 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa miezi mitatu.

3 Mfalme wa Misri akamwondoa madarakani huko Yerusalemu na akatoza Yuda kodi ya talanta 100za fedha na talanta mojaya dhahabu.

4 Mfalme wa Misri akamweka Eliyakimu, nduguye Yehoahazi, kuwa mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu na kubadili jina la Eliyakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini Neko akamchukua Yehoahazi, Nduguye Eliyakimu akampeleka Misri.

Yehoyakimu Mfalme Wa Yuda

5 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni paBwanaMungu wake.

6 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli.

7 Nebukadneza akachukua pia vyombo kutoka katika Hekalu laBwanana kuviweka katika hekalu lakehuko Babeli.

8 Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu, machukizo aliyoyafanya na yote yaliyoonekana dhidi yake, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Yehoyakimu mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.

9 Yehoyakimu alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi. Akafanya yaliyo maovu machoni paBwana.

10 Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka katika Hekalu laBwananaye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.

Mfalme Sedekia Wa Yuda

11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa muda wa miaka kumi na mmoja.

12 Akafanya yaliyo maovu machoni paBwanaMungu wake wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno laBwana.

13 Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukiaBwana, Mungu wa Israeli.

14 Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu laBwanaalilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.

Kuanguka Kwa Yerusalemu

15 Bwana, Mungu wa baba zao, akawapelekea neno kupitia wajumbe wake tena na tena, kwa sababu alikuwa anawahurumia watu wake pamoja na mahali pa maskani yake.

16 Lakini waliwadhihaki wajumbe waBwanawakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu yaBwanaikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza.

17 Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.

18 Akavichukua kwenda Babeli vyombo vyote kutoka katika Hekalu la Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za Hekalu laBwanapamoja na hazina za mfalme na za maafisa wake.

19 Wakalitia moto Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani.

20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, nao wakawa watumishi wake na wa wanawe mpaka wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi.

21 Nchi ikaendelea kufurahia pumziko lake la Sabato, wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika mpaka ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno laBwanalililonenwa na Yeremia.

Koreshi Atangaza Uhuru Kwa Waliokuwa Uhamishoni

22 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili litimie lile neno laBwanalililosemwa na nabii Yeremia,Bwanaakausukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutoa tangazo kwa maandishi katika utawala wake wote:

23 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, huyo mtu na apande.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2CH/36-a1021885c5760e6e2e55b215f5fd4a01.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

19 + 13 =