2 Samweli 22

Wimbo Wa Daudi Wa Sifa

1 Daudi akamwimbiaBwanamaneno ya wimbo huu hapoBwanaalipomwokoa kutoka katika mkono wa adui zake wote, pia kutoka katika mkono wa Sauli.

2 Akasema:

“Bwanani mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

3 Mungu wangu ni mwamba wangu,

ambaye kwake nakimbilia,

ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.

Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu

na mwokozi wangu,

huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

4 NamwitaBwana, yeye anayestahili kusifiwa,

nami ninaokolewa

kutoka kwa adui zangu.

5 “Mawimbi ya mauti yalinizunguka,

maji mengi ya ghafula

ya uharibifu yalinifunika.

6 Kamba za kuzimuzilinizunguka,

mitego ya kifo ilinikabili.

7 Katika shida yangu nilimwitaBwana,

nilimwita Mungu wangu.

Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,

kilio changu kikafika masikioni mwake.

8 “Dunia ilitetemeka na kutikisika,

misingi ya mbingu ilitikisika,

vilitetemeka kwa sababu

alikuwa amekasirika.

9 Moshi ukapanda kutoka puani mwake,

moto ulao ukatoka kinywani mwake,

makaa ya moto yawakayo kwa nguvu

yalitoka humo.

10 Akazipasua mbingu akashuka chini,

mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

11 Alipanda juu ya kerubi akaruka,

akapaa juu kwa mbawa za upepo.

12 Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika:

mawingu meusi ya mvua ya angani.

13 Kutokana na mng’ao wa uwepo wake

mawingu yalisogea,

ikanyesha mvua ya mawe

na umeme wa radi.

14 Bwanaalinguruma kutoka mbinguni,

sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

15 Aliipiga mishale akatawanya adui,

umeme wa radi na kuwakimbiza.

16 Mabonde ya bahari yalifunuliwa

na misingi ya dunia ikawa wazi

kwa kukaripia kwakeBwana,

kwa uvumi wa pumzi

kutoka puani mwake.

17 “Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;

alinitoa kutoka katika kilindi

cha maji makuu.

18 Aliniokoa kutoka mtesi wangu

mwenye nguvu nyingi,

kutoka adui zangu, waliokuwa na nguvu

nyingi kuliko mimi.

19 Walinikabili katika siku ya msiba wangu,

lakiniBwanaalikuwa msaada wangu.

20 Alinileta nje mahali penye nafasi tele,

akaniokoa kwa sababu alipendezwa nami.

21 “Bwanaalinitendea kwa kadiri ya uadilifu wangu;

kwa kadiri ya usafi wa mikono yangu amenilipa.

22 Kwa maana nimezishika njia zaBwana

sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

23 Sheria zake zote zi mbele yangu,

wala sijayaacha maagizo yake.

24 Nimekuwa sina hatia mbele zake,

nami nimejilinda nisitende dhambi.

25 Bwanaamenilipa sawa sawa na uadilifu wangu,

sawa sawa na usafi wangu machoni pake.

26 “Kwa yeye aliye mwaminifu

unajionyesha kuwa mwaminifu,

kwa asiye na hatia unajionyesha

kuwa asiye na hatia,

27 kwa aliye mtakatifu

unajionyesha kuwa mtakatifu,

lakini kwa aliyepotoka

unajionyesha kuwa mkaidi.

28 Wewe huwaokoa wanyenyekevu,

lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi

ili uwashushe.

29 Wewe ni taa yangu, EeBwana.

Bwanahulifanya giza langu

kuwa mwanga.

30 Kwa msaada wako naweza kusogeza jeshi,

nikiwa pamoja na Mungu wangu

nitaweza kuruka.

31 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu;

neno laBwanani kamilifu.

Yeye ni ngao kwa wote

wanaokimbilia kwake.

32 Kwa maana ni nani aliye Mungu

zaidi yaBwana?

Ni nani aliye Mwamba

isipokuwa Mungu wetu?

33 Mungu ndiye anivikaye nguvu

na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

34 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,

huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

35 Huifundisha mikono yangu kwa ajili ya kupigana vita;

mikono yangu inaweza kupinda upindi wa shaba.

36 Hunipa ngao yako ya ushindi,

hujishusha chini ili kuniinua.

37 Huyapanua mapito yangu,

ili vifundo vya miguu yangu visipinduke.

38 “Nilifuatia adui zangu na nikawaseta;

sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

39 Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka;

walianguka chini ya miguu yangu.

40 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;

uliwafanya adui zangu

kusujudu miguuni pangu.

41 Uliwafanya adui zangu wageuke na wakakimbia,

nami nikawaangamiza adui zangu.

42 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na ye yote wa kuwaokoa;

walimliliaBwana, lakini hakuwajibu.

43 Niliwapiga wakawa laini kama mavumbi ya nchi;

nikawaponda na kuwakanyaga

kama tope barabarani.

44 “Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu;

umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa.

Watu ambao sikuwajua wananitumikia,

45 nao wageni huja wakininyenyekea;

mara wanisikiapo, hunitii.

46 Wote hulegea;

huja wakitetemeka

kutoka kwenye ngome zao.

47 “Bwanayu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!

Atukuzwe Mungu,

Mwamba, Mwokozi wangu!

48 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,

ayawekaye mataifa chini yangu,

49 aniwekaye huru toka kwa adui zangu.

Uliniinua juu ya adui zangu;

uliniokoa toka kwa watu wajeuri.

50 Kwa hiyo nitakusifu wewe, EeBwana,

katikati ya mataifa;

nitaliimbia sifa jina lako.

51 Humpa mfalme wake ushindi mkuu;

huonyesha fadhili zake

kwa mpakwa mafuta wake,

kwa Daudi na wazao wake milele.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2SA/22-29f734b8edeca81bc9fa9c69b32334a4.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seventeen + 11 =