2 Samweli 23

Maneno Ya Mwisho Ya Daudi

1 Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi:

“Neno la Daudi mwana wa Yese,

neno la mtu aliyeinuliwa na Aliye Juu Sana,

mtu aliyepakwa mafuta na Mungu wa Yakobo,

mwimbaji wa nyimbo wa Israeli:

2 “Roho waBwanaalinena kupitia kwangu,

neno lake lilikuwa ulimini mwangu.

3 Mungu wa Israeli alinena,

mwamba wa Israeli akaniambia:

‘Mtu anatawala watu kwa haki,

wakati anapotawala

akiwa na hofu ya Mungu,

4 yeye ni kama mwanga wa asubuhi jua lichomozapo

asubuhi isiyo na mawingu,

kama mwanga baada ya mvua

uchipuzao majani kutoka ardhini.’

5 “Je, si hivyo ilivyo nyumba yangu

mbele za Mungu?

Je, hajafanya Agano la milele nami,

lililopangwa na kuimarishwa

kila sehemu?

Je, hatanifanya niufurahie wokovu wangu

na kunijalia matakwa yangu yote?

6 Lakini watu waovu wote

watatupwa kando kama miiba,

ambayo haikusanywi kwa mkono.

7 Ye yote agusaye miiba

hutumia chombo cha chuma

au mpini wa mkuki,

nayo huchomwa pale ilipo.”

Mashujaa Wa Daudi

8 Haya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:

# Yosheb-Bashebethi, Mtahkemoni, alikuwa ndiye kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua kwa siku moja.

9 Wa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai, Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati walipowadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,

10 lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga.Bwanaakawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

11 Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia.

12 Lakini Shama akasimama imara katikati ya shamba. Akatetea na kuwaua Wafilisti, nayeBwanaakawapatia ushindi mkubwa.

13 Wakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati ambapo kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi kufika Bonde la Refaimu.

14 Wakati huo Daudi alikuwa ndani ya ngome, nao askari walinzi wa ngome wa Wafilisti walikuwa huko Bethlehemu.

15 Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti kama mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kile kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!”

16 Basi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwenye kile kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu na kumletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa; badala yake, aliyamimina mbele zaBwana.

17 Akasema, “Iwe mbali nami, EeBwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa.

Haya yalifanywa na hao mashujaa watatu.

18 Abishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye aliyekuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.

19 Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuwekwa miongoni mwao.

20 Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabzeeli, ambaye alifanya mambo mengi ya ushujaa. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni siku kulipokuwa na barafu na kumwuua simba.

21 Pia alimwua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumwua kwa mkuki wake mwenyewe.

22 Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu sawa na wale mashujaa watatu.

23 Alipata heshima kubwa zaidi kuliko ye yote wa wale Thelathini, lakini hakuwekwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi alimweka kuwa kiongozi wa walinzi wake mwenyewe.

24 Miongoni mwa wale Thelathini walikuwepo:

Asaheli ndugu wa Yoabu;

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;

25 Shama, Mharodi;

Elika, Mharodi;

26 Helesi, Mpalti;

Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;

27 Abiezeri kutoka Anathothi;

Mebunai, Mhushathi;

28 Salmoni, Mwahohi;

Muharai, Mnetofathi;

29 Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi;

Ithai mwana wa Ribai kutoka Gibea katika Benyamini;

30 Benaya, Mpirathoni;

Hidai kutoka vijito vya Gaashi;

31 Abi-Alboni, Mwarbathi;

Azmawethi, Mbarhumi;

32 Eliaba, Mshaalboni;

wana wa Yasheni;

Yonathani

33 mwana wa Shama, Mharari;

Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;

34 Elifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi;

Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

35 Hezro, Mkarmeli;

Paarai, Mwarbi;

36 Igali mwana wa Nathani kutoka Soba;

mwana wa Hagri;

37 Seleki, Mwaamori;

Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mchukuzi wa silaha za Yoabu mwana wa Seruya;

38 Ira, Mwithri;

Gerebu, Mwithri;

39 na Uria, Mhiti.

Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2SA/23-1c34637ed3ddd6c0e20b9a7fc9ee6bca.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

1 + 12 =