2 Wafalme 2

Eliya Achukuliwa Juu Mbinguni

1 WakatiBwanaalipokuwa karibu kumchukua Eliya juu mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya na Elisha walikuwa njiani kutoka Gilgali.

2 Eliya akamwambia Elisha, “Kaa hapa,Bwanaamenituma Betheli.”

Lakini Elisha akasema, “Kwa hakika, kamaBwanaaishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo wakaenda Betheli pamoja.

3 Wana wa manabii walikuwako huko Betheli wakamjia Elisha na kumwuliza, “Je, unajua ya kwambaBwanaatakuondolea bwana wako leo?”

Elisha akawajibu, “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”

4 Kisha Eliya akamwambia, “Baki hapa Elisha,Bwanaamenituma Yeriko.”

Naye akajibu, “Kwa hakika kamaBwanaaishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.

5 Wana wa manabii waliokuwako huko Yeriko wakamwendea Elisha na kumwuliza, “Je, unajua ya kwambaBwanaatakuondolea bwana wako leo?”

Akawajibu “Ndiyo, najua, lakini msizungumze juu ya jambo hilo.”

6 Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa,Bwanaamenituma kwenda Yordani.”

Naye akamjibu, “Kwa hakika kamaBwanaaishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wote wawili wakaendelea pamoja.

7 Wana hamsini wa manabii wakaenda na kusimama kwa mbali, kuelekea mahali ambapo Eliya na Elisha walikuwa wamesimama katika Mto Yordani.

8 Eliya akachukua vazi lake, akalisokota na kupiga nalo maji. Maji yakagawanyika upande wa kuume na upande wa kushoto, nao wawili wakavuka pakavu.

9 Walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, “Niambie, nikufanyie nini kabla sijaondolewa kutoka kwako?”

Elisha akajibu, “Naomba nirithi sehemu maradufu ya roho yako.”

10 Eliya akasema, “Umeomba jambo gumu, lakini kama utaniona wakati ninapoondolewa kutoka kwako litakuwa lako, la sivyo, haitakuwa hivyo.”

11 Walipokuwa wakitembea pamoja na kuzungumza, ghafula gari la moto na farasi wa moto vilitokea na kuwatenganisha wao wawili, naye Eliya akapanda mbinguni katika upepo wa kisulisuli.

12 Elisha aliona hili akapaza sauti, “Baba yangu! Baba yangu! Magari ya Israeli na wapanda farasi wake!” Naye Elisha hakumwona tena. Kisha akazishika nguo zake mwenyewe na kuzichana.

13 Akaliokota lile vazi lililoanguka kutoka kwa Eliya, kisha akarudi na kusimama ukingoni mwa Yordani.

14 Ndipo akalichukua lile vazi ambalo lilikuwa limeanguka kutoka kwa Eliya naye akayapiga nalo yale maji. Akauliza, “Yuko wapi sasaBwana, Mungu wa Eliya?” Alipoyapiga maji, yakagawanyika kulia na kushoto, naye akavuka.

15 Wale wana wa manabii kutoka Yeriko, waliokuwa wakitazama, wakasema, “Roho wa Eliya inamkalia Elisha.” Nao wakaenda kumlaki na kusujudu hadi nchi mbele yake.

16 Wakasema, “Tazama, sisi watumishi wako tunao watu hamsini wenye uwezo. Waruhusu waende kumtafuta bwana wako. Labda Roho waBwanaamemtwaa na kumweka katika mlima fulani au bonde fulani.”

Elisha akajibu, “Hapana, msiwatume.”

17 Lakini wakasisitiza mpaka akaona aibu kuwakatalia. Hivyo akasema, “Watumeni.” Nao wakawatuma watu hamsini, wakamtafuta kwa siku tatu, lakini hawakumpata.

18 Walipomrudia Elisha, ambaye alikuwa akingojea huko Yeriko, akawaambia, “Je, sikuwaambia msiende?”

Kuponywa Kwa Maji

19 Watu wa mji wakamwambia Elisha, “Tazama, bwana wetu, mahali mji huu ulipojengwa ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo, lakini maji yake ni mabaya na nchi haizai.”

20 Akasema, “Nileteeni bakuli mpya, wekeni chumvi ndani yake.” Kwa hiyo wakamletea.

21 Kisha akatoka akaenda kwenye chemchemi na kuitupa ile chumvi ndani yake, akisema, “Hili ndilo asemaloBwana: ‘Nimeyaponya maji haya. Kamwe hayatasababisha mauti tena wala kutozaa.’ ”

22 Nayo yale maji yakaponywa mpaka leo, sawasawa na neno la Elisha alilokuwa amesema.

Elisha Anafanyiwa Mzaha

23 Kutoka huko Elisha akakwea kwenda Betheli. Ikawa alipokuwa akitembea barabarani, baadhi ya vijana wakatoka mjini na kumfanyia mzaha. Wakisema, “Paa, wewe mwenye upaa! Paa, wewe mwenye upaa!”

24 Akageuka, akawatazama na kuwalaani kwa Jina laBwana. Kisha dubu wawili wa kike wakatokea mwituni na kuwararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao.

25 Naye akaondoka huko akaenda Mlima Karmeli, na kutoka huko akarudi Samaria.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2KI/2-a89796c5c49ac9f07ac2aa8492a598f5.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − eight =