Ayubu 2

Jaribu La Pili La Ayubu

1 Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele zaBwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake.

2 Bwanaakamwuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibuBwana“Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

3 Bwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Mtu ambaye hakuna mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado mpaka sasa anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

4 Shetani akajibu, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake.

5 Lakini nyosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

6 Bwanaakamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umuachie uhai wake.”

7 Basi Shetani akatoka mbele zaBwananaye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.

8 Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

9 Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

10 Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavuye yote angelinena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

11 Basi marafiki watatu wa Ayubu, Elifazi, Mtemani na Bildadi, Mshuhi na Sofari, Mnaamathi waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka majumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.

12 Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua, wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao.

13 Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba mchana na usiku. Hakuna ye yote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/2-fc6d18042f3d3806c85f9523944f0fb0.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

fourteen + 10 =