Ayubu 23

Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu

1 Ndipo Ayubu akajibu:

2 “Hata leo malalamiko yangu ni uchungu,

mkono wake ni mzito juu yangu

pamoja na kulia kwangu kwa uchungu.

3 Laiti ningefahamu mahali pa kumwona,

laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!

4 Ningeliweka shauri langu mbele zake

na kukijaza kinywa changu na hoja.

5 Ningejua kwamba angenijibu nini

na kuelewa lile ambalo angelisema.

6 Je, angenipinga kwa nguvu nyingi?

La, asingenigandamiza, bali angenisikiliza.

7 Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,

nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.

8 “Lakini nikienda mashariki, hayupo,

nikienda magharibi, simpati.

9 Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni,

akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.

10 Lakini anaijua njia niiendeayo,

akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.

11 Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu,

nimeishika njia yake bila kukengeuka.

12 Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake,

bali nimeyathamini maneno ya kinywa chake

kuliko chakula changu cha kila siku.

13 “Lakini yeye ndiye aamuaye peke yake,

ni nani awezaye kumpinga?

Yeye hufanya lo lote alitakalo.

14 Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,

na bado anayo mipango mingi kama hiyo

ambayo ameiweka akiba.

15 Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake,

nifikiriapo haya yote ninamwogopa.

16 Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia,

yeye Mwenyezi amenitia hofu.

17 Hata hivyo sikunyamazishwa na giza,

wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOB/23-141a9b0fd288b09e7b73418d07072958.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 + twelve =