Ezekieli 14

Waabudu Sanamu Walaumiwa

1 Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu.

2 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

3 “Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lo lote?

4 Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli ye yote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, MimiBwananitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu.

5 Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.

6 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!

7 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimiBwananitamjibu mwenyewe.

8 Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumwadibisha ili wengine waonywe na kumfanya kitu cha kudharauliwa na watu. Nitamkatilia mbali kutoka katika watu wangu. Ndipo mtakapojua Mimi ndimiBwana.

9 “ ‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, MimiBwananitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli.

10 Watachukua hatia yao, nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake.

11 “ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Ndipo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

Hukumu Isiyoepukika

12 Neno laBwanalikanijia kusema,

13 “Mwanadamu, kama nchi itanitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikinyoosha mkono wangu dhidi yake kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao,

14 hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Yobu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asemaBwanaMwenyezi.

15 “Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori,

16 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa.

17 “Au kama nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikiua watu wake na wanyama wao,

18 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.

19 “Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao,

20 hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Yobu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.

21 “Kwa maana hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao!

22 Lakini watakuwepo wenye kuokoka, wana na binti wataletwa kutoka nje ya nchi hiyo. Watawajia ninyi, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya yale yote niliyoleta juu yake.

23 Mtafarijika wakati mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwa kuwa mtajua kwamba sikufanya lo lote ndani yake bila sababu, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/14-2d309217ba3a2dfec287a73d3c9427ee.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven − 2 =