Ezekieli 30

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,

“Ole wa siku ile!”

3 Kwa kuwa siku ile imekaribia,

siku yaBwanaimekaribia,

siku ya mawingu,

siku ya maangamizi kwa mataifa.

4 Upanga utakuja dhidi ya Misri,

nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.

Mauaji yatakapoangukia Misri,

utajiri wake utachukuliwa

na misingi yake itabomolewa.

5 Kushina Putu, Ludi na Arabia yote, Libyana watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

6 “ ‘Hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka

na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.

Kutoka Migdoli hadi Aswani,

watauawa ndani yake kwa upanga,

asemaBwanaMwenyezi.

7 “ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa

miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,

nayo miji yao itakuwa magofu

miongoni mwa miji iliyo magofu.

8 Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimiBwana,

nitakapoiwasha Misri moto

na wote wamsaidiao watapondwa.

9 “ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

10 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri

kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,

litaletwa ili kuangamiza nchi.

Watafuta panga zao dhidi ya Misri

na kuijaza nchi kwa waliouawa.

12 Nitakausha vijito vya Nile

na nitaiuza nchi kwa watu waovu,

kwa mkono wa wageni,

nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu

kilichomo ndani yake.

MimiBwananimenena haya.

13 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu

# na kukomesha vinyago katika Memfisi.

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,

nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

14 Nitaifanya Pathrosikuwa ukiwa

na kuitia moto Soani,

# nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi.

15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,

ngome ya Misri,

nami nitakatilia mbali

makundi ya wajeuri wa Thebesi.

16 Nitaitia moto nchi ya Misri;

Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.

Thebesi itachukuliwa na tufani,

Memfisi itakuwa katika taabu daima.

17 Wanaume vijana wa Onina wa Pi-Besethi

wataanguka kwa upanga

nayo hiyo miji itatekwa.

18 Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza

nitakapovunja kongwa la Misri;

hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.

Atafunikwa na mawingu

na vijiji vyake vitatekwa.

19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,

nao watajua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno laBwanalikanijia kusema:

21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.

22 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake.

23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huko na huko katika nchi zote.

24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha.

25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyosha dhidi ya Misri.

26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huko na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZK/30-1df7d03bab06f06833e454751ecfd504.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 3 =