Hesabu 8

Kuwekwa Kwa Taa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ”

3 Aroni akafanya hivyo; akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

4 Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambachoBwanaalikuwa amemwonyesha Mose.

Kutengwa Kwa Walawi Kwa Ajili Ya Bwana

5 Bwanaakamwambia Mose:

6 “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada.

7 Ili kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe.

8 Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

9 Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli.

10 Utawaleta Walawi mbele zaBwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.

11 Aroni atawaweka Walawi mbele zaBwanakama sadaka ya kupunga kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi yaBwana.

12 “Baada ya Walawi kuweka mikono yao juu ya vichwa vya hao mafahali wawili, tumia mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi kwaBwana, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.

13 Waambie hao Walawi wasimame mbele ya Aroni na wanawe, kisha wawatoe kama sadaka ya kupunga kwaBwana.

14 Kwa njia hii utakuwa umewatenga Walawi kutoka Waisraeli wengine, nao Walawi watakuwa wangu.

15 “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kupunga, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania.

16 Wao ndio Waisraeli ambao watatolewa kabisa kwangu. Nimewatwaa kama mali yangu mwenyewe badala ya mzaliwa wa kwanza, mzaliwa wa kwanza wa kiume kutoka kwa kila mwanamke wa Kiisraeli.

17 Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume katika Israeli, awe wa mwanadamu au mnyama, ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wote wa kwanza huko Misri, niliwatenga kwa ajili yangu mwenyewe.

18 Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa kiume katika Israeli.

19 Kati ya Waisraeli wote, nimempa Aroni na wanawe Walawi kama zawadi ili wafanye kazi katika Hema la Kukutania kwa niaba ya Waisraeli, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili pasiwepo na pigo lo lote litakalowapata Waisraeli wakati watakapokaribia mahali patakatifu.”

20 Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli wakawafanyia Walawi kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

21 Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Aroni akawasogeza mbele zaBwanakuwa sadaka ya kupunga, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.

22 Baada ya hayo, Walawi walikuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania chini ya usimamizi wa Aroni na wanawe. Waliwafanyia Walawi kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

23 Bwanaakamwambia Mose,

24 “Hili linawahusu Walawi: Wanaume wenye umri wa miaka ishirini na mitano au zaidi watakuja kushiriki katika kazi kwenye Hema la Kukutania,

25 lakini watakapofika umri wa miaka hamsini, ni lazima waache kazi zao za kawaida wala wasiendelee.

26 Wanaweza kuwasaidia ndugu zao kufanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, lakini wao wenyewe kamwe hawatafanya hiyo kazi. Basi, hivi ndivyo utakavyogawa wajibu kwa Walawi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/8-9c3b2beda352a25ba9fadd06a50575b1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × five =