Hesabu 9

Pasaka Huko Sinai

1 Bwanaakasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema,

2 “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamuriwa.

3 Adhimisheni wakati ulioamuriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

4 Hivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka,

5 nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

6 Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Mose na Aroni siku ile ile,

7 wakamwambia Mose, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtoleaBwanasadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamuriwa?”

8 Mose akawajibu, “Ngojeni mpaka nitafute kileBwanaanachoagiza kuwahusu ninyi.”

9 NdipoBwanaakamwambia Mose,

10 “Waambie Waisraeli: ‘Wakati mmoja wenu au wazao wenu wanapokuwa najisi kwa sababu ya maiti au wakiwa safarini, hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka yaBwana.

11 Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu.

12 Wasibakize cho chote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote.

13 Lakini kama mtu ni safi kwa taratibu za kiibada naye hayuko safarini asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake kwa sababu hakutoa sadaka yaBwanakwa wakati ulioamuriwa. Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake.

14 “ ‘Mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka yaBwana, lazima afanye hivyo kwa kufuata desturi na masharti. Lazima masharti yawe sawasawa kwa mgeni na mzawa.’ ”

Wingu La Moto Juu Ya Maskani

15 Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, liliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya maskani lilionekana kama moto.

16 Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto.

17 Wakati wo wote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali po pote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi.

18 Kwa amri yaBwanaWaisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.

19 Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri yaBwananao hawakuondoka.

20 Wakati mwingine wingu lilikuwa juu ya Maskani kwa siku chache tu; kwa amri yaBwanawangelipiga kambi na kisha kwa amri yake wangeliondoka.

21 Wakati mwingine wingu lilikuwapo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wo wote wingu lilipoinuka, waliondoka.

22 Ikiwa wingu lilikaa juu ya Maskani kwa siku mbili au mwezi au mwaka, Waisraeli wangebaki wamepiga kambi na hawakuondoka; lakini lilipoinuka, wangeondoka.

23 Kwa amri yaBwanawalipiga kambi, na kwa amri yaBwanawaliondoka. Walitii amri yaBwana, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NUM/9-befe803cce6de1a5d4676487a0b545ea.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven − six =