Hosea 1

1 Neno laBwanalililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yekoashi mfalme wa Israeli:

Mke Wa Hosea Na Watoto

2 WakatiBwanaalipoanza kuzungumza kupitia Hosea,Bwanaalimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwachaBwana.”

3 Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana.

4 KishaBwanaakamwambia Hosea, “Mwite Yezreeli, kwa kuwa kitambo kidogo nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa ajili ya mauaji ya kule Yezreeli, nami nitaukomesha ufalme wa Israeli.

5 Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.”

6 Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. KishaBwanaakamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama, kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe.

7 Hata hivyo nitaonyesha upendo kwa nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa si kwa upinde, upanga au vita, wala kwa farasi na wapanda farasi, bali kwa njia yaBwanaMungu wao.”

8 Baada ya Gomeri kumwachisha Lo-Ruhama kunyonya, Gomeri alipata mwana mwingine.

9 KishaBwanaakasema, “Mwite Lo-Amikwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.

10 “Hata hivyo Waisraeli watakuwa kama mchanga kando ya bahari, ambao hauwezi kupimika wala kuhesabiwa. Mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’

11 Watu wa Yuda na watu wa Israeli wataunganishwa tena, nao watamchagua kiongozi mmoja nao watakwea watoke katika nchi, kwa kuwa siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/HOS/1-3c0b99c1b9b82448541b0fa16862dcd1.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

7 + 20 =