Yoeli 3

Mataifa Yahukumiwa

1 “Katika siku hizo na wakati huo,

nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,

2 nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta

# katika Bonde la Yehoshafati.

Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao

kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli,

kwa kuwa waliwatawanya watu wangu

miongoni mwa mataifa

na kuigawa nchi yangu.

3 Wanawapigia kura watu wangu

na kuwauza wavulana ili kupata makahaba;

waliwauza wasichana

ili wapate kunywa mvinyo.

4 “Sasa una nini dhidi yangu, Ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda.

5 Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu.

6 Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.

7 “Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya.

8 Nitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Washeba, taifa lililo mbali.”Bwanaamesema.

9 Tangazeni hili miongoni mwa mataifa:

Jiandaeni kwa vita!

Amsha askari!

Wanaume wote wapiganaji

wasogee karibu na kushambulia.

10 Majembe yenu yafueni yawe panga

na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.

Aliye dhaifu na aseme,

“Mimi nina nguvu!”

11 Njoni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,

kusanyikeni huko.

Shusha wapiganaji wako, EeBwana!

12 “Mataifa na yaamshwe;

na yasonge mbele kuelekea katika Bonde la Yehoshafati,

kwa kuwa nitaketi mahali pale

kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

13 Tia mundu,

kwa kuwa mavuno yamekomaa.

Njoni, mkanyage zabibu,

kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa

na mapipa yanafurika:

kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”

14 Umati mkubwa, umati mkubwa

katika bonde la uamuzi!

Kwa kuwa siku yaBwanani karibu

katika bonde la uamuzi.

15 Jua na mwezi vitatiwa giza,

na nyota hazitatoa mwanga wake tena.

16 Bwanaatanguruma kutoka Sayuni

na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;

dunia na mbingu vitatikisika.

LakiniBwanaatakuwa kimbilio la watu wake,

ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.

Baraka Kwa Watu Wa Mungu

17 “Ndipo mtakapojua kwamba Mimi,BwanaMungu wenu,

nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

Yerusalemu utakuwa mtakatifu;

kamwe wageni hawataivamia tena.

18 “Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,

na vilima vitatiririka maziwa;

mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.

Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba yaBwana

# na kunywesha Bonde la Shitimu.

19 Lakini Misri itakuwa ukiwa,

Edomu itakuwa jangwa tupu,

kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,

ambao katika nchi yao

walimwaga damu isiyo na hatia.

20 Yuda itakaliwa na watu milele

na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

21 Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe,

nitasamehe.”

Bwanaanakaa Sayuni!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JOL/3-8663e10b8d72a40fd5193aeae4bf422a.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × 4 =