Isaya 66

Hukumu Na Matumaini

1 Hili ndilo asemaloBwana,

“Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Iko wapi nyumba mtakayojenga kwa ajili yangu?

Mahali pangu pa kupumzika patakuwa wapi?

2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?”

asemaBwana.

“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

3 Lakini ye yote atoaye dhabihu ya fahali

ni kama yeye auaye mtu,

na ye yote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,

ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa;

ye yote atoaye sadaka ya nafaka,

ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,

na ye yote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,

ni kama yule aabuduye sanamu.

Wamejichagulia njia zao wenyewe,

nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao,

4 hivyo, mimi pia nitachagua mapigo makali kwa ajili yao,

nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.

Kwa maana nilipoita, hakuna ye yote aliyejibu,

niliposema, hakuna ye yote aliyesikiliza.

Walifanya maovu machoni pangu

na kuchagua lile linalonichukiza.”

5 Sikieni neno laBwana,

ninyi mtetemekao kwa neno lake,

“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi

na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,

‘Bwanana atukuzwe,

ili tupate kuona furaha yenu!’

Hata sasa wataaibika.

6 Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,

sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!

Ni sauti yaBwanaikiwalipa adui zake

yote wanayostahili.

7 “Kabla hajasikia utungu, alizaa;

kabla hajapata maumivu,

alizaa mtoto mwanaume.

8 Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?

Ni nani amepata kuona mambo kama haya?

Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja

au taifa laweza kutokea mara?

Mara Sayuni alipoona utungu,

alizaa watoto wake.

9 Je, nilete hadi wakati wa kuzaliwa

na nisizalishe?” asemaBwana.

“Je, nifunge tumbo la uzazi

wakati mimi ndiye nizalishaye?”

asema Mungu wako.

10 “Shangilieni pamoja na Yerusalemu

na mfurahi kwa ajili yake,

ninyi nyote mnaompenda,

shangilieni kwa nguvu pamoja naye,

ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka

katika faraja ya matiti yake;

mtakunywa sana,

na kuufurahia wingi wa mafuriko

ya ustawi wake.”

12 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana:

“Nitamwongezea amani kama mto,

nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho,

utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake

na kubembelezwa magotini pake.

13 Kama mama anavyomfariji mtoto wake,

ndivyo nitakavyokufariji wewe,

nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

14 Wakati mtakapoona jambo hili,

mioyo yenu itashangilia,

nanyi mtastawi kama majani;

mkono waBwanautajulikana kwa watumishi wake,

bali ghadhabu yake kali

itaonyeshwa kwa adui zake.

15 Tazama,Bwanaanakuja na moto,

magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,

atatelemsha hasira yake kwa ghadhabu kali

na karipio lake pamoja na miali ya moto.

16 Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake

Bwanaatatekeleza hukumu juu ya watu wote,

nao wengi watakuwa ni wale

waliouawa naBwana.

17 “Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asemaBwana.

18 “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.

19 “Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Putuna Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.

20 Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka katika mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwaBwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asemaBwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu laBwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.

21 Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asemaBwana.

22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asemaBwana, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu.

23 Kutoka Mwezi Mpya hata Mwezi Mpya mwingine na kutoka Sabato hadi Sabato nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asemaBwana.

24 “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi, funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ISA/66-d36be496ce49a45a4cc727d8e05ba436.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two + fourteen =