Kumbukumbu La Torati 10

Vibao Vingine Vya Amri Kumi

1 Wakati uleBwanaaliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao.

2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”

3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu.

4 Bwanaakaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko.Bwanaakanikabidhi.

5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kamaBwanaalivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

6 (Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eliezeri mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani.

7 Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji.

8 Wakati huoBwanaaliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano laBwana, kusimama mbele zaBwanaili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo.

9 Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kamaBwanaMungu wao alivyowaambia.)

10 Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini mchana na usiku, kama nilivyofanya mara ya kwanza, piaBwanaalinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza.

11 Bwanaakaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”

Mche Bwana

12 Na sasa, Ee Israeli,BwanaMungu wako anataka nini kwako ila kumchaBwanaMungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikiaBwanaMungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,

13 na kuyashika maagizo yaBwanana amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali yaBwanaMungu wako.

15 Hata hivyoBwanaalikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.

16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

17 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.

18 Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

19 Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri.

20 McheBwanaMungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.

21 Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.

22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasaBwanaMungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/10-ef0829b15dd02672c90a099b6e3f50fb.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × three =