Kumbukumbu La Torati 9

Si Kwa Sababu Ya Haki Ya Waisraeli

1 Sikiliza, Ee Israeli. Sasa mnakaribia kuvuka Yordani mwingie na kuwafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi pamoja na miji mikubwa yenye kuta zilizofika juu angani.

2 Watu ni wenye nguvu na warefu, ni wana wa Waanaki! Mnafahamu habari zao na mmesikia inavyosemekana: “Ni nani awezaye kusimama dhidi ya Waanaki?”

3 Iweni na hakika leo kwambaBwanaMungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kamaBwanaalivyowaahidi.

4 Baada yaBwanaMungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Bwanaametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya kwambaBwanaanawafukuza mbele yenu.

5 Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya,BwanaMungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.

6 Basi mjue, si kwa sababu ya haki yenuBwanaMungu wenu anawapa nchi hii nzuri kuimiliki, kwa kuwa ninyi ni taifa lenye shingo ngumu.

Ndama Ya Dhahabu

7 Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirishaBwanaMungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi yaBwana.

8 Kule Horebu mliamsha ghadhabu yaBwana, kwa hiyo alikasirika vya kutosha hata akataka kuwaangamiza.

9 Nilipopanda mlimani kupokea mbao za mawe, mbao za Agano lileBwanaalilofanya nanyi, nilikaa mlimani siku arobaini mchana na usiku, sikula mkate wala sikunywa maji.

10 Bwanaalinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu. Juu ya mbao hizo kulikuwapo amri zote ambazoBwanaaliwatangazieni kule mlimani kwa njia ya moto, siku ya kusanyiko.

11 Mwisho wa siku arobaini mchana na usiku,Bwanaalinipa mbao mbili za mawe, mbao za Agano.

12 KishaBwanaakaniambia, “Shuka chini mara moja, kwa sababu watu wako ambao umewatoa katika nchi ya Misri wamepotoka. Wamegeukia mbali haraka kutoka lile nililowaagiza, wamejitengenezea sanamu ya kusubu.”

13 NayeBwanaakaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana!

14 Niache, ili nipate kuwaangamiza na kufuta jina lao kutoka chini ya mbingu. Nami nitakufanya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwa wengi kuliko wao.”

15 Kwa hiyo niligeuka na kutelemka kutoka mlimani kwani mlima ulikuwa ukiwaka moto. Pia vibao vile viwili vya Agano vilikuwa mikononi mwangu.

16 Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ileBwanaaliyowaagiza.

17 Kwa hiyo nilichukua vibao vile viwili nikavitupa na kuvipasua vipande vipande mbele ya macho yenu.

18 Ndipo tena nikasujudu mbele zaBwanakwa siku arobaini mchana na usiku. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele zaBwanana kumkasirisha.

19 Niliogopa hasira na ghadhabu yaBwana, kwa kuwa aliwakasirikia vya kutosha na kutaka kuwaangamiza. LakiniBwanaalinisikiliza tena.

20 Bali yeye alimkasirikia Aroni kiasi cha kutaka kumwangamiza, nami wakati huo nilimwombea Aroni pia.

21 Kisha nikachukua ile sanamu ya ndama mliyoitengeneza na kuichoma kwenye moto. Nikaiponda na kuisaga ikawa unga laini kama vumbi, nikatupa lile vumbi kwenye kijito kilichotiririka toka mlimani.

22 Pia mlimkasirishaBwanahuko Tebera, Masa na Kibroth-Hataava.

23 Vile vile wakatiBwanaalipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimekwisha wapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo laBwanaMungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii.

24 Mmekuwa waasi dhidi yaBwanatangu nilipowajua ninyi.

25 Nilianguka kifudifudi mbele zaBwanakwa zile siku arobaini mchana na usiku kwa sababuBwanaalikuwa amesema angewaangamiza ninyi.

26 NilimwombaBwanana kusema, “EeBwanaMwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.

27 Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.

28 Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababuBwanahakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’

29 Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/DEU/9-f6f1a5dcfb89326722970806253438ff.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seventeen + one =