Malaki 3

1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo.

3 Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha, atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. KishaBwanaatakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki,

4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwaBwana, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, nao wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

Kumwibia Mungu

6 “MimiBwanasibadiliki. Kwa hiyo ninyi, Enyi uzao wa Yakobo, hamjaangamizwa.

7 Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

8 “Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

“Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

“Mnaniibia zaka na dhabihu.

9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha au la.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

13 “Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asemaBwana.

“Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’

14 “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele zaBwanaMwenye Nguvu Zote?

15 Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”

16 Ndipo wale waliomchaBwanawakasemezana wao kwa wao, nayeBwanaakasikiliza naye akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimchaBwanana kuliheshimu jina lake.

17 “Nao watakuwa watu wangu,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia.

18 Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/3-e12e85093aad32613aefd604cc373f9f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 − eleven =