Malaki 4

Siku Ya Bwana

1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.

2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

3 Kisha ninyi mtawakanyaga waovu nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 “Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

5 “Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha yaBwana.

6 Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/MAL/4-5240a62128de639eb6ba1d9251f8fc90.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × one =