Mambo ya Walawi 17

Kunywa Damu Kumekatazwa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Aroni na wanawe pamoja na Waisraeli wote uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaaliloagiza:

3 Mwisraeli ye yote atakayetoa dhabihu ya maksai, mwana-kondoo au mbuzi ndani ya kambi au nje yake,

4 badala ya kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kuileta kama sadaka kwaBwanambele ya Maskani yaBwana, mtu huyo atahesabiwa kuwa na hatia ya kumwaga damu; ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

5 Hii ni ili kwamba Waisraeli wamleteeBwanadhabihu wanazozifanya sasa mahali pa wazi mashambani. Ni lazima wazilete kwa makuhani, yaani kwaBwana, katika ingilio la Hema la Kukutania na kutoa dhabihu kama sadaka za amani.

6 Kuhani atanyunyiza damu kwenye madhabahu yaBwanakatika ingilio la Hema la Kukutania na kuyateketeza mafuta ya hiyo dhabihu kuwa harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

7 Hawatatoa kamwe dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi ambazo wamekuwa wakijifanyia nazo ukahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwao na kwa ajili ya vizazi vijavyo.’

8 “Waambie: ‘Mwisraeli ye yote au mgeni ye yote anayeishi miongoni mwao atakayetoa sadaka ya kuteketezwa au dhabihu

9 bila kuileta kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili kutoa dhabihu kwaBwana, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

10 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi miongoni mwao ambaye hunywa damu yo yote, nitakuwa kinyume cha mtu huyo atakayekunywa damu na kumkatilia mbali na watu wake.

11 Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu, nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu; damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu.

12 Kwa hiyo, ninawaambia Waisraeli, “Hakuna hata mmoja wenu anayeruhusiwa kunywa damu, wala mgeni anayeishi miongoni mwenu haruhusiwi kunywa damu.”

13 “ ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye atamwinda mnyama au ndege anayeruhusiwa kuliwa ni lazima aimwage damu na kuifunika kwa udongo,

14 kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake. Ndiyo sababu nimewaambia Waisraeli, “Kamwe msinywe damu ya kiumbe cho chote, kwa sababu uhai wa kila kiumbe ni katika damu yake; ye yote atakayekunywa damu ni lazima akatiliwe mbali.”

15 “ ‘Mtu ye yote, awe mzaliwa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu cho chote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi.

16 Lakini kama hakufua nguo zake na kuoga, atakuwa na hatia kwa kosa hilo.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/17-aaca7b63fca635cd053bb6e26c56a0de.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − eleven =