Mambo ya Walawi 21

Sheria Kwa Ajili Ya Makuhani

1 Bwanaakamwambia Mose, “Sema na makuhani, wana wa Aroni, uwaambie: ‘Kwa utaratibu wa kiibada kamwe kuhani asijitie unajisi kwa ajili ya kugusa maiti ya mtu wake ye yote,

2 isipokuwa maiti ya jamaa yake wa karibu, kama vile mama yake au baba yake, mwanawe au binti yake, ndugu yake,

3 au dada yake asiyeolewa ambaye anamtegemea kwa kuwa hana mume, kwa ajili ya hao aweza kugusa maiti na kujitia unajisi.

4 Kamwe asijitie unajisi mwenyewe kutokana na wale watu ambao anahusiana nao kwa kuoana, na hivyo kujitia unajisi.

5 “ ‘Kamwe makuhani wasinyoe nywele za vichwa vyao wala wasinyoe pembeni mwa ndevu zao au kuweka chale kwenye miili yao.

6 Lazima wawe watakatifu kwa Mungu wao na kamwe wasilinajisi jina la Mungu wao. Kwa sababu ndio wanaotoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kwaBwana, chakula cha Mungu wao, hivyo lazima wawe watakatifu.

7 “ ‘Kamwe wasioe wanawake waliojinajisi kwa ukahaba au waliopewa talaka na waume wao, kwa sababu makuhani ni watakatifu kwa Mungu wao.

8 Waoneni kuwa watakatifu, kwa sababu ndio wanaotoa chakula cha Mungu wenu. Kumbukeni kuwa ni watakatifu, kwa sababu MimiBwanani mtakatifu, Mimi niwafanyaye ninyi watakatifu.

9 “ ‘Ikiwa binti wa kuhani amejitia unajisi kwa kufanya ukahaba, anamwaibisha baba yake; lazima achomwe kwa moto.

10 “ ‘Kuhani mkuu, aliye miongoni mwa ndugu zake, ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa wala asirarue nguo zake.

11 Kamwe asiingie ndani mahali penye maiti. Kamwe asijitie unajisi, hata kwa ajili ya baba yake au mama yake,

12 wala asiondoke mahali patakatifu pa Mungu wake au kupanajisi, kwa sababu amewekwa wakfu kwa kupakwa mafuta ya Mungu wake. Mimi ndimiBwana.

13 “ ‘Mwanamke atakayemwoa ni lazima awe bikira.

14 Kamwe asimwoe mjane, au mwanamke aliyepewa talaka, wala mwanamke aliyejinajisi kwa ukahaba, bali atamwoa tu bikira kutoka miongoni mwa watu wake,

15 hivyo hatawatia unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. Mimi ndimiBwana, nimfanyaye mtakatifu.’ ”

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Mwambie Aroni: ‘Kwa vizazi vijavyo hakuna mzao wako mwenye dosari atakayekaribia kutoa chakula cha Mungu wake.

18 Hakuna mtu mwenye dosari yo yote awezaye kukaribia: hakuna mtu aliye kipofu au kiwete, au aliyeharibika uso au asiye na viungo kamili,

19 hakuna mtu mwenye mguu au mkono uliolemaa,

20 au mwenye kibiongo au aliyedumaa, au aliye na tatizo la macho, au aliye na uvimbe wenye usaha au majipu, au aliyehasiwa.

21 Hakuna mzao wa kuhani Aroni mwenye kilema cho chote atakayekaribia kutoa sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto. Kama ana kilema, kamwe asikaribie kutoa chakula cha Mungu wake.

22 Anaweza kula chakula kitakatifu sana cha Mungu wake, pia hata chakula kitakatifu;

23 lakini kwa sababu ya kilema chake, kamwe asikaribie karibu na pazia wala kukaribia madhabahu, asije akanajisi mahali patakatifu pangu. Mimi ndimiBwana, niwafanyaye watakatifu.’ ”

24 Basi Mose akamwambia Aroni jambo hili na wanawe pamoja na Waisraeli wote.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/21-0f25e6a1e915580ef462ca08f53b4909.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twenty − 4 =