Mambo ya Walawi 22

Matumizi Ya Sadaka Takatifu

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Mwambie Aroni na wanawe kushughulikia kwa uangalifu sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwangu, ili wasilinajisi Jina langu takatifu. Mimi ndimiBwana.

3 “Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa ye yote wa wazao wako ni najisi kwa taratibu za kiibada, naye akakaribia sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwaBwana, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimiBwana.

4 “ ‘Ikiwa mzao wa Aroni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Vile vile atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu cho chote kilichotiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,

5 au ikiwa atagusa kitu cho chote kitambaacho hicho kimfanyacho mtu najisi, au mtu ye yote awezaye kumtia unajisi, unajisi uwao wote.

6 Mtu anayegusa kitu cho chote cha aina hiyo atakuwa najisi mpaka jioni. Kamwe hatakula sadaka yo yote takatifu mpaka yeye mwenyewe awe ameoga kwa maji.

7 Wakati jua linapotua, atakuwa safi na baada ya hilo anaweza kula sadaka takatifu, kwa kuwa ni vyakula vyake.

8 Kamwe asile nyama ya mzoga wala iliyoraruliwa na wanyama pori, naye akatiwa unajisi kwa hilo. Mimi ndimiBwana.

9 “ ‘Makuhani lazima washike maagizo yangu ili wasiwe na hatia, wakafa kwa kuyadharau. Mimi ndimiBwananinayewafanya watakatifu.

10 “ ‘Hakuna mtu ye yote asiye wa jamaa ya kuhani anayeruhusiwa kula sadaka takatifu, wala mgeni wa kuhani au mfanyakazi wake haruhusiwi kuila.

11 Lakini ikiwa kuhani amenunua mtumwa kwa fedha, au mtumwa amezaliwa katika nyumba ya kuhani huyo, mtumwa huyo aweza kula chakula cha huyo kuhani.

12 Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, binti huyo haruhusiwi kula cho chote cha matoleo matakatifu.

13 Lakini ikiwa binti wa kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, naye akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula cho chote katika chakula hiki.

14 “ ‘Ikiwa mtu ye yote amekula sadaka takatifu kwa makosa, lazima atoe malipo ya sadaka hiyo kwa kuhani na kuongeza sehemu ya tano ya thamani ya sadaka hiyo.

15 Kamwe makuhani wasiinajisi sadaka takatifu ambayo Waisraeli wameitoa kwaBwana

16 kwa kuwaruhusu kuzila sadaka hizo takatifu, na hivyo kuwaletea hatia ya kudaiwa malipo. Mimi ndimiBwananiwafanyaye watakatifu.’ ”

Dhabihu Zisizokubalika

17 Bwanaakamwambia Mose,

18 “Sema na Aroni, wanawe na Waisraeli wote na uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwaBwana, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari,

19 lazima mtoe mnyama dume asiye na dosari akiwa ng’ombe, mbuzi au kondoo ili kwamba aweze kukubalika kwa niaba yako.

20 Kamwe usitoe kitu cho chote chenye dosari kwa sababu hakitakubaliwa kwa niaba yako.

21 Mtu ye yote aletapo sadaka ya amani kwaBwanakutoka kundi la ng’ombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.

22 Kamwe usimtoleeBwanamnyama aliye kipofu, aliyejeruhiwa wala aliye kilema, au cho chote kilicho na uvimbe, au chenye upele au vidonda vinavyotoka usaha. Kamwe cho chote cha aina hii kisiwekwe juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto.

23 Pengine, waweza kuamua na ukatoa sadaka ya hiari ng’ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa, lakini hii haitakubalika ili kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.

24 Kamwe usimtoleeBwanamnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au aliyehasiwa, au yaliyoraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye katika nchi yako mwenyewe,

25 na kamwe usikubali wanyama wa aina hii kutoka katika mkono wa mgeni na kuwatoa wanyama hao kuwa chakula kwa Mungu wako. Wanyama hao hawatakubaliwa kwa niaba yako, kwa sababu wana vilema, nao wana dosari.’ ”

26 Bwanaakamwambia Mose,

27 “Wakati ndama, mwana-kondoo au mwana-mbuzi azaliwapo, atabaki na mama yake kwa siku saba. Kuanzia siku ya nane na kuendelea anaweza kukubaliwa kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.

28 Usimchinje ng’ombe na ndama wake, au kondoo na kitoto chake siku moja.

29 “UnapomtoleaBwanadhabihu ya shukrani, itoe kwa namna ambayo itakubalika kwa niaba yako.

30 Ni lazima iliwe siku iyo hiyo, pasipo kubakiza cho chote mpaka asubuhi. Mimi ndimiBwana.

31 “Shikeni maagizo yangu na kuyafuata. Mimi ndimiBwana.

32 Msilinajisi Jina langu takatifu. Lazima nikubalike kuwa mtakatifu kwa Waisraeli. Mimi ndimiBwananinayewafanya watakatifu

33 na niliyewatoa katika nchi ya Misri niwe Mungu wenu. Mimi ndimiBwana.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/LEV/22-cfb2ab300106a4582dcaa9f85ce6e717.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

6 + two =