Nehemiah 8

1 watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja kwenye uwanja mbele ya Lango la Maji. Wakamwambia Ezra mwandishi alete kitabu cha sheria ya Mose, ambachoBwanaaliamuru kwa ajili ya Israeli.

2 Basi katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba kuhani Ezra akaleta Sheria mbele ya kusanyiko, ambamo walikuwemo wanaume, wanawake na watu wote walioweza kufahamu.

3 Akaisoma kwa sauti kubwa tangu mapambazuko mpaka adhuhuri akiwa ameuelekea uwanja uliokuwa mbele ya Lango la Maji mbele ya wanaume, wanawake na wengine ambao waliweza kufahamu. Watu wote wakasikiliza kwa makini kile Kitabu cha Sheria.

4 Mwandishi Ezra akasimama juu ya jukwaa la miti lililojengwa kwa kusudi hilo. Karibu naye upande wa kuume alisimama Matithia, Shema, Anaya, Uria, Hilkia na Maaseya. Upande wake wa kushoto walikuwepo Pedaya, Mishaeli, Malkiya, Hashumu, Hashbadani, Zekaria na Meshulamu.

5 Ezra akakifungua kile kitabu. Watu wote waliweza kumwona kwa sababu alikuwa amesimama juu zaidi, naye alipokifungua watu wote wakasimama.

6 Ezra akamsifuBwana, Mungu mkuu, nao watu wote wakainua mikono yao na kuitikia, “Amen! Amen!” Kisha wakasujudu na kumwabuduBwanahali nyuso zao zikigusa ardhi.

7 Wakati wakiwa wamesimama pale walawi wafuatao walikuwa wakiwaelewesha watu ile sheria: Yeshua, Bani, Sherebia, Jamini, Akubu, Shabethai, Hodai, Maaseya, Kelita, Azaria, Yozabadi, Hanani na Pelaya.

8 Walisoma kutoka katika kile Kitabu cha Sheria ya Mungu, wakiifafanua na kuwapa maelezo ili watu waweze kufahamu kile kilichokuwa kikisomwa.

9 Kwa kuwa watu wote walikuwa wakilia walipokuwa wakisikiliza maneno ya ile Sheria. Ndipo Nehemia Tirshatha, Ezra kuhani na mwandishi, pamoja na Walawi waliokuwa wakiwafundisha watu wakawaambia wote, “Siku hii ni takatifu kwaBwanaMungu wenu. Msiomboleze wala msilie.”

10 Nehemia akasema, “Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana cho chote cha kula. Siku hii ni takatifu kwaBwana. Msihuzunike, kwa kuwa furaha yaBwanani nguvu zenu.”

11 Walawi wakawatuliza watu wote wakisema, “Iweni watulivu, kwa kuwa hii ni siku takatifu. Msihuzunike.”

12 Kisha watu wote wakaondoka kwenda kula na kunywa na kuwapelekea watu sehemu ya chakula na wakaadhimisha kwa furaha kubwa, kwa sababu sasa wamefahamu maneno yale waliyokuwa wameelezwa.

13 Katika siku ya pili ya mwezi, wakuu wa mbari zote, pamoja na makuhani na Walawi, walikusanyika wakimzunguka Ezra mwandishi wapate kusikiliza kwa makini maneno ya Sheria.

14 Wakakuta imeandikwa katika ile Sheria, ambayoBwanaaliiamuru kupitia kwa Mose kwamba Waisraeli wanapaswa kukaa katika vibanda wakati wa sikukuu ya mwezi wa saba

15 na kwamba wanapaswa kutangaza neno hili na kulieneza katika miji yao na katika Yerusalemu wakisema: “Enendeni katika nchi ya mlima na kuleta matawi kutoka miti ya mizeituni, mizeituni mwitu, mihadasi, mitende na miti ya kivuli, ili kutengeneza vibanda,” kama ilivyoandikwa.

16 Basi watu wakaenda na kuleta matawi nao wakajijengea vibanda juu ya paa za nyumba zao, katika nyua zao, katika nyua za nyumba ya Mungu na katika uwanja karibu na Lango la Maji na uwanja wa Lango la Efraimu.

17 Jamii yote ya watu waliorudi kutoka utumwani wakajenga vibanda na kuishi ndani yake. Tangu wakati wa Yoshua mwana wa Nuni mpaka siku ile, Waisraeli hawakuwahi kuiadhimisha namna hii kama hivi. Furaha yao ilikuwa kubwa sana.

18 Siku baada ya siku, kuanzia siku ya kwanza hadi ya mwisho, Ezra alisoma kutoka kwenye kile Kitabu cha Sheria ya Mungu. Wakaadhimisha sikukuu ile kwa siku saba na katika siku ya nane, kwa kufuatana na maagizo, kulikuwa na kusanyiko maalum.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/NEH/8-e97364f016c37ffeccd1c00d2f62fb16.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

3 × three =