Yeremia 22

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

1 Hili ndilo asemaloBwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na utangaze ujumbe huu huko:

2 ‘Sikia neno laBwana, Ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi, wewe, maafisa wako na watu wako mnaokuja kwa kupitia malango haya.

3 Hili ndiloBwanaasemalo: Tenda kwa haki na kwa adili. Mwokoe kutoka mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane wal a usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

4 Kwa kuwa kama ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao.

5 Lakini kama hukuyatii maagizo haya, asemaBwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

6 Kwa kuwa hili ndiloBwanaasemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,

kama kilele cha Lebanoni,

hakika nitakufanya uwe kama jangwa,

kama miji ambayo haijakaliwa na watu.

7 Nitawatuma waharabu dhidi yako,

kila mtu akiwa na silaha zake,

nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi

na kuzitupa motoni.

8 “Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa niniBwanaamefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’

9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha Agano laBwana, Mungu wao na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

10 Usimlilie yeye aliyekufa wala usimwombolezee;

badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu

yule aliyepelekwa uhamishoni,

kwa sababu kamwe hatairudia

wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

11 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwanakuhusu Shalumumwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “yeye kamwe hatarudi tena.

12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka, hataiona tena nchi hii.”

13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme

kwa njia ya dhuluma,

vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,

akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,

bila kuwalipa kwa utumushi wao.

14 Asemaye, ‘Nitajijengea jumba kubwa la kifalme

na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’

Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,

huweka mbao za mierezi

na kuipamba kwa rangi nyekundu.

15 “Je, inakufanya kuwa mfalme

kwa kuongeza idadi ya mierezi?

Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?

Alifanya yaliyo sawa na haki,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

16 Aliwatetea maskini na wahitaji,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote,

Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”

asemaBwana.

17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

katika mapato ya udhalimu,

kwa kumwaga damu isiyo na hatia,

kwa uonevu na ukatili.”

18 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanakuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

“Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, ndugu yangu! Ole umbu langu!’

Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

19 Atazikwa maziko ya punda:

ataburutwa na kutupwa

nje ya malango ya Yerusalemu.”

20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,

sauti yako na isikike huko Bashani,

piga kelele toka Abarimu, kwa kuwa

wale wote waliojiunga nawe

wameangamizwa.

21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’

Hii imekuwa ndiyo kawaida yako tangu ujana wako;

hujanitii mimi.

22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

wale ulioungana nao

watakwenda uhamishoni.

Kisha utaaibika na kufedheheka kwa sababu

ya uovu wako wote.

23 Wewe uishiye Lebanoni,

wewe uliyetulia

kwenye majengo ya mierezi,

tazama jinsi utakavyoomboleza

maumivu makali yatakapokupata,

maumivu kama yale ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa!

24 “Hakika kama niishivyo,” asemaBwana, “hata kama wewe, Yekoniamwana wa Yehoyakimumfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekung’oa utoke hapo.

25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.

26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.

27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

28 Je, huyu Yekonia ni mtu aliyedharauliwa,

chungu kilichovunjika,

tena chombo kisichotakiwa na mtu ye yote?

Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,

na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

29 Ee nchi, nchi, nchi,

sikia neno laBwana!

30 Hili ndiloBwanaasemalo:

“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,

mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,

kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,

kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi

wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/22-44564e86e85d800cc764660656ea5d8f.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

14 − 6 =