Yeremia 21

Mungu Anakataa Ombi La Sedekia

1 Neno lilimjia Yeremia kutoka kwaBwanawakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake kusema:

2 “Tuulizie sasa kwaBwanakwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. LabdaBwanaatatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita ili Nebukadneza atuondokee.”

3 Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia,

4 ‘Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.

5 Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi.

6 Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha.

7 Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga, hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asemaBwana.

8 “Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima na njia ya mauti.

9 Ye yote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini ye yote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi atanusurika, naye ataishi.

10 Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza kwa moto, asemaBwana.’

11 “Zaidi ya hayo, iambie nyumba ya kifalme ya Yuda, ‘Sikia neno laBwana,

12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

Mwokoeni kutoka mikononi mwa mdhalimu

yeye aliyetekwa nyara,

la sivyo ghadhabu yangu italipuka

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mlioufanya:

itawaka na hakuna wa kuizima.

13 Niko kinyume nawe, Ee Yerusalemu,

wewe uishiye juu ya bonde hili

kwenye uwanda wa juu wa miamba,

asemaBwana,

wewe usemaye, “Ni nani awezaye

kuja kinyume chetu?

Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”

14 Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu,

asemaBwana.

Nitawasha moto katika misitu yenu

ambao utateketeza kila kitu

kinachowazunguka ninyi.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/21-98eb96f08aac4f2dc1e604a1079c9c98.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 8 =