Yeremia 27

Yuda Kumtumikia Nebukadneza

1 Mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwaBwana:

2 Hili ndiloBwanaaliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako uifunge kwa kamba za ngozi.

3 Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.

4 Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Waambieni hivi mabwana zenu:

5 Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa ye yote inipendezavyo.

6 Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nitawafanya hata wanyama wa mwituni wamtumikie.

7 Mataifa yote yatamtumikia yeye pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.

8 “ ‘ “Lakini kama kukiwa na taifa lo lote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asemaBwana, mpaka nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake.

9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.’

10 Wanawatabiria ninyi uongo ambako kutawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka kwenye nchi yenu, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia.

11 Lakini ikiwa taifa lo lote litainama na kuweka shingo yake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asemaBwana.” ’ ”

12 Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, mtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi.

13 Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni ambayoBwanaameonya juu ya taifa lo lote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?

14 Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo.

15 ‘Sikuwatuma hao,’ asemaBwana. ‘Wanatabiri uongo kwa Jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”

16 Kisha nikawaambia makuhani na watu wote hawa, “Hili ndilo asemaloBwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba yaBwanavitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.

17 Ninyi msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?

18 Kama wao ni manabii na wanalo neno laBwana, basi na wamsihiBwanaMwenye Nguvu Zote kwamba vyombo vilivyobaki katika nyumba yaBwanana katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.

19 Kwa maana hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,

20 ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.

21 Naam, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba yaBwanana ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu:

22 ‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asemaBwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha tena mahali hapa.’ ”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/27-22fef31aa57262e873068fe74e6163b2.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × two =