Yeremia 28

Hanania Nabii Wa Uongo

1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba yaBwanambele ya makuhani na watu wote:

2 “Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.

3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba yaBwanaambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.

4 Pia nitamrudisha mahali hapa Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walikwenda Babeli,’ asemaBwana, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ”

5 Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba yaBwana.

6 Akasema, “Amen!Bwanana afanye hivyo!Bwanana ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba yaBwanapamoja na wote waliohamishwa.

7 Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote:

8 Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.

9 Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa naBwanaikiwa unabii wake utatimia.”

10 Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,

11 naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemaloBwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Kwa jambo hili, nabii Yeremia akaondoka zake.

12 Kitambo kidogo baada nabii Hanania kuivunja nira kutoka katika shingo ya nabii Yeremia, neno laBwanalikamjia Yeremia:

13 “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma.

14 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”

15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania!Bwanahajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.

16 Kwa hiyo, hili ndilo asemaloBwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi yaBwana.’ ”

17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JER/28-3413058eee3e7851ec5f1108be449b17.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + 1 =