Yona 4

Hasira ya Yona Kwa Ajili ya Huruma ya Bwana.

1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika.

2 AkamwombaBwana, “EeBwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.

3 Sasa, EeBwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

4 LakiniBwanaakamjibu, “Je unayo haki yo yote kukasirika?”

5 Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.

6 NdipoBwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpatia Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu.

7 Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka.

8 Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

9 Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?”

Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”

10 LakiniBwanaakamwambia, “Wewe waona vibaya kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja nao ukafa usiku mmoja.

11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto pamoja na ng’ombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/JON/4-da616231ce885d25d27bec5b3a1c64da.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

seven + twelve =