Zaburi 1

Furaha Ya Kweli

1 Heri mtu yule ambaye

haendi katika shauri la watu waovu,

wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi

au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

2 Bali huifurahia sheria yaBwana,

naye huitafakari hiyo sheria mchana na usiku.

3 Mtu huyo ni kama mti uliopandwa

kando ya vijito vya maji,

ambao huzaa matunda kwa majira yake

na majani yake hayanyauki.

Lo lote afanyalo hufanikiwa.

Huzuni Ya Waovu

4 Sivyo walivyo waovu!

Wao ni kama makapi

yapeperushwayo na upepo.

5 Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,

wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

6 Kwa maanaBwanahuziangalia njia za mwenye haki,

bali njia ya waovu itaangamia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/1-461588185b7df957126ca69dd341074d.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

thirteen − 5 =