Zaburi 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu

(Zaburi Ya Daudi)

1 EeBwana, ninakuita wewe,

uje kwangu hima.

Sikia sauti yangu ninapokuita.

2 Maombi yangu na yafike mbele zako

kama uvumba;

kuinua mikono yangu juu

na kuwe kama dhabihu ya jioni.

3 EeBwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4 Usiuache moyo wangu uvutwe katika lililo baya,

nisije nikashiriki katika matendo maovu

pamoja na watu watendao mabaya,

wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

5 Mtu mwenye haki na anipige:

ni jambo la huruma;

na anikemee,

ni mafuta kichwani mwangu.

Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima

ni kinyume cha watenda mabaya,

6 watawala wao watatupwa chini

kutoka kwenye majabali,

waovu watajifunza kwamba maneno yangu

yalikuwa kweli.

7 Watasema, “Kama mtu anavyolima

na kuvunja ardhi,

ndivyo mifupa yetu imetawanywa

kwenye mlango wa kaburi.”

8 Lakini nimekaza macho yangu kwako,

EeBwanaMwenyezi,

ndani yako nimekimbilia,

usiniache nife.

9 Niepushe na mitego waliyonitegea,

kutokana na mitego

iliyotegwa na watenda mabaya.

10 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,

wakati mimi ninapita salama.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/141-2e78f72da3c85efe3c132cabfafda772.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

15 − five =