Zaburi 18

Wimbo Wa Daudi Wa Ushindi

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi Mtumishi Wa Mungu Aliyomwimbia Mungu Wakati Mungu Alipomwokoa Mkononi Mwa Sauli Na Adui Wengine)

1 Nakupenda wewe, EeBwana,

nguvu yangu.

2 Bwanani mwamba wangu,

ngome yangu na mwokozi wangu,

Mungu wangu ni mwamba,

ambaye kwake ninakimbilia.

Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu,

ngome yangu.

3 NinamwitaBwanaanayestahili kusifiwa,

nami nimeokoka kutoka kwa adui zangu.

4 Kamba za mauti zilinizunguka,

mafuriko ya maangamizi yalinilemea.

5 Kamba za kuzimu zilinizunguka,

mitego ya mauti ilinikabili.

6 Katika shida yangu nalimwitaBwana,

nilimlilia Mungu wangu anisaidie.

Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu,

kilio changu kikafika mbele zake,

masikioni mwake.

7 Dunia ikatetemeka na kutikisika,

misingi ya milima ikayumbayumba,

ilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

8 Pua zake zilitoa moshi,

moto uteketezao ulitoka kinywani mwake,

makaa ya moto yawakayo

yakatoka ndani mwake.

9 Alizipasua mbingu akashuka chini,

mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

10 Alipanda kerubi akaruka,

akapaa juu kwa mbawa za upepo.

11 Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,

chandarua chake kumzunguka,

mawingu meusi ya mvua angani.

12 Kutokana na mwanga mkali wa uwepo wake

mawingu yalisogea,

ikanyesha mvua ya mawe

na umeme wa radi.

13 Bwanaalinguruma kutoka mbinguni,

sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

14 Aliipiga mishale yake na kutawanya adui,

naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

15 EeBwana, kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako,

sakafu ya bahari ikaonekana,

misingi ya dunia ikawa wazi.

16 Akanyosha mkono wake kutoka juu, akanishika,

akanitoa kutoka katika maji mengi.

17 Akaniokoa kutoka adui yangu mwenye nguvu nyingi,

kutoka adui zangu,

waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.

18 Walinishambulia siku ya taabu yangu,

lakiniBwanaalikuwa msaada wangu.

19 Alinileta nje mahali penye nafasi tele,

akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.

20 Bwanaalinitendea sawa sawa na uadilifu wangu;

sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.

21 Kwa maana nimezishika njia zaBwana,

sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.

22 Sheria zake zote zi mbele yangu,

wala sijayaacha maagizo yake.

23 Nimekuwa sina hatia mbele zake,

nami nimejilinda nisitende dhambi.

24 Bwanaamenilipa sawasawa na uadilifu wangu;

sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake.

25 Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu,

kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia.

26 Kwa aliye safi unajionyesha kuwa safi,

lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.

27 Wewe huwaokoa wanyenyekevu

lakini huwashusha wenye kiburi.

28 Wewe, EeBwana, unaifanya taa yangu

iendelee kuwaka,

Mungu wangu hulifanya giza langu

kuwa mwanga.

29 Kwa msaada wako nitashinda jeshi,

nikiwa pamoja na Mungu wangu

nitaweza kuruka ukuta.

30 Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu,

neno laBwanani kamili.

Yeye ni ngao kwa wote

wanaokimbilia kwake.

31 Kwa maana ni nani aliye Mungu

zaidi yaBwana?

Ni nani aliye Mwamba

isipokuwa Mungu wetu?

32 Mungu ndiye anivikaye nguvu na

kufanya njia yangu kuwa kamilifu.

33 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,

huniwezesha kusimama mahali palipo juu.

34 Huifundisha mikono yangu kupigana vita,

mikono yangu inaweza

kupinda upinde wa shaba.

35 Hunipa ngao yako ya ushindi,

mkono wako wa kuume hunitegemeza,

huinama chini ili kuniinua.

36 Hupanua mapito yangu,

ili miguu yangu isiteleze.

37 Niliwafuatia adui zangu na nikawapata,

sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

38 Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena,

walianguka chini ya miguu yangu.

39 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita,

adui zangu uliwafanya wasujudu miguuni pangu.

40 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,

nami nikawaangamiza adui zangu.

41 Walipiga yowe kuomba msaada,

lakini hapakuwepo na ye yote wa kuwaokoa;

walimliliaBwana, lakini hakuwajibu.

42 Niliwaponda wakawa kama mavumbi

yanayopeperushwa na upepo,

nikawamwaga nje kama tope barabarani.

43 Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu;

umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa,

watu ambao sikuwajua wananitumikia.

44 Mara wanisikiapo hunitii,

wageni hunyenyekea mbele yangu.

45 Wote wanalegea,

wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.

46 Bwanayu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!

Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!

47 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,

awatiishaye mataifa chini yangu,

48 aniokoaye na adui zangu.

Uliniinua juu ya adui zangu;

uliniokoa toka watu wajeuri.

49 Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, EeBwana;

nitaliimbia sifa jina lako.

50 Humpa mfalme wake ushindi mkuu,

huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,

kwa Daudi na uzao wake milele.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/18-0f64b340122b4c9189b542d8db0ea1a7.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 + 2 =