Zaburi 19

Utukufu Wa Mungu Katika Uumbaji

(Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi)

1 Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu,

anga zahubiri kazi ya mikono yake.

2 Siku baada ya siku zinatoa habari,

usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

3 Hakuna msemo wala lugha,

ambapo sauti zao hazisikiki.

4 Sauti yao imeenea duniani pote,

maneno yao yameenea

mpaka miisho ya dunia.

Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,

5 linafanana na bwana arusi

akitoka chumbani mwake,

kama shujaa afurahiavyo

kukamilisha kushindana kwake.

6 Huchomoza upande mmoja wa mbingu,

na kufanya mzunguko wake

hadi upande mwingine,

hakuna kilichojificha joto lake.

7 Sheria yaBwanani kamilifu,

ikihuisha nafsi.

Shuhuda zaBwanani za kuaminika,

zikimpa mjinga hekima.

8 Maagizo yaBwanani kamili,

nayo hufurahisha moyo.

Amri zaBwanahuangaza,

zatia nuru machoni.

9 KumchaBwanani utakatifu,

nako kwadumu milele.

Amri zaBwanani za hakika,

nazo zina haki.

10 Ni za thamani kuliko dhahabu,

kuliko dhahabu iliyo safi sana,

ni tamu kuliko asali,

kuliko asali kutoka kwenye sega.

11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,

katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

12 Ni nani awezaye kutambua makosa yake?

Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.

13 Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi,

nazo zisinitawale.

Ndipo nitakapokuwa sina lawama,

wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

14 Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu,

yapate kibali mbele zako,

EeBwana, Mwamba wangu

na Mkombozi wangu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/19-9f11ab7437be115ca6c824090f37be77.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × 1 =