Zaburi 25

Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi

(Zaburi Ya Daudi)

1 Kwako wewe, EeBwana,

nainua nafsi yangu,

2 ni wewe ninayekutumainia,

Ee Mungu wangu.

Usiniache niaibike,

wala usiache adui zangu wakanishinda.

3 Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea

atakayeaibishwa,

bali wataaibishwa wafanyao hila

bila sababu.

4 Nionyeshe njia zako, EeBwana,

nifundishe mapito yako,

5 niongoze katika kweli yako na kunifundisha,

kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,

nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

6 Kumbuka, EeBwana,

rehema zako kuu na upendo,

kwa maana zimekuwapo tangu zamani.

7 Usizikumbuke dhambi za ujana wangu

wala njia zangu za uasi,

sawasawa na upendo wako unikumbuke,

kwa maana wewe ni mwema, EeBwana.

8 Bwanani mwema na mwenye adili,

kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.

9 Huwaongoza wanyenyekevu katika haki,

naye huwafundisha njia yake.

10 Njia zote zaBwanani za upendo na aminifu

kwa wale wanaoshika Agano na shuhuda zake.

11 EeBwana, kwa ajili ya jina lako,

unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.

12 Ni nani basi, mtu yule anayemchaBwana?

Atamfundisha katika njia

atakayoichagua kwa ajili yake.

13 Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake,

nao wazao wake watairithi nchi.

14 Siri yaBwanaiko kwa wale wamchao,

yeye huwajulisha Agano lake.

15 Macho yangu humwelekeaBwanadaima,

kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa

miguu yangu kutoka katika mtego.

16 Nigeukie na unihurumie, kwa maana mimi

ni mpweke na mwenye kuteseka.

17 Shida za moyo wangu zimeongezeka,

niokoe kutoka katika dhiki yangu.

18 Uangalie mateso na shida zangu

na uniondolee dhambi zangu zote.

19 Tazama adui zangu walivyo wengi,

pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!

20 Uyalinde maisha yangu na uniokoe,

usiniache niaibike,

kwa maana nimekukimbilia wewe.

21 Uadilifu na uaminifu vinilinde,

kwa sababu tumaini langu ni kwako.

22 Ee Mungu, mkomboe Israeli,

kutoka katika shida zake zote!

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/25-d574a817dbd54a3e276411792368f1c6.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × 4 =