Zaburi 28

Kuomba Msaada

(Zaburi Ya Daudi)

1 Ninakuita wewe, EeBwana, Mwamba wangu;

usiwe kwangu kama kiziwi.

Kwa sababu ukinyamaza

nitafanana na hao

waliokwisha shuka shimoni.

2 Sikia kilio changu unihurumie

ninapokuita kwa ajili ya msaada,

niinuapo mikono yangu kuelekea

Patakatifu pa Patakatifu pako.

3 Usiniburute pamoja na waovu,

pamoja na hao watendao mabaya,

ambao huzungumza na jirani zao

maneno mazuri,

lakini mioyoni mwao wameficha chuki.

4 Uwalipe sawasawa na matendo yao,

sawasawa na matendo yao maovu;

walipe sawasawa na kazi za mikono yao,

uwalipe wanavyostahili.

5 Kwa kuwa hawaheshimu kazi zaBwana,

na yale ambayo mikono yake imetenda,

atawabomoa na kamwe

hatawajenga tena.

6 Bwanaasifiwe,

kwa maana amesikia kilio changu

nikimwomba anihurumie.

7 Bwanani nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

8 Bwanani nguvu ya watu wake,

ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.

9 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako;

uwe mchungaji wao na uwabebe milele.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/28-ccdd4c1f15c10ab12f79c0f60d9b93a3.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen − eleven =