Zekaria 10

Bwana Ataitunza Yuda

1 MwombeniBwanamvua wakati wa vuli;

ndiyeBwanaatengenezaye mawingu ya tufani.

Huwapa watu manyunyu ya mvua,

pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

2 Sanamu huzungumza udanganyifu,

waaguzi huona maono ya uongo;

husimulia ndoto ambazo si za kweli,

wanatoa faraja batili.

Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo

walioonewa kwa kukosa mchungaji.

3 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,

nami nitawaadhibu viongozi;

kwa kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote

atalichunga kundi lake,

nyumba ya Yuda,

naye atawafanya kuwa kama farasi

mwenye kiburi akiwa vitani.

4 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,

kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,

kutoka kwake utatoka upinde wa vita,

kutoka kwake atatoka kila mtawala.

5 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa

wanaokanyaga barabara za matope

wakati wa vita.

Kwa sababuBwanayu pamoja nao,

watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

6 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimiBwanaMungu wao,

nami nitawajibu.

7 Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.

Watoto wao wataona na kufurahi,

mioyo yao itashangilia katikaBwana.

8 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.

Hakika nitawakomboa,

nao watakuwa wengi

kama walivyokuwa mwanzoni.

9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,

hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali

watanikumbuka mimi.

Wao na watoto wao watanusurika katika hatari

nao watarudi.

10 Nitawarudisha kutoka Misri

na kuwakusanya toka Ashuru.

Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,

na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

11 Watapita katika bahari ya mateso;

bahari iliyochafuka itatulizwa

na vilindi vyote vya Mto Nile vitakauka.

Kiburi cha Ashuru kitashushwa,

nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

12 Nitawaimarisha katikaBwana,

na katika jina lake watatembea,”

asemaBwana.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/10-7ec337ae9edf5ebc6d71d1068febb350.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 + six =