Zekaria 9

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

Neno

1 Neno laBwanaliko kinyume na nchi ya Hadraki

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,

kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote

za Israeli yako kwaBwana,

2 pia juu ya Hamathi inayopakana nayo,

juu ya Tiro na Sidoni,

ingawa wana ujuzi mwingi sana.

3 Tiro amejijengea ngome imara,

amelundika fedha kama mavumbi

na dhahabu kama taka za mitaani.

4 Lakini Bwana atamwondolea mali zake

na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

naye atateketezwa kwa moto.

5 Ashkeloni ataona hili na kuogopa;

Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,

pia Ekroni, kwa sababu

matumaini yake yatanyauka.

Gaza atampoteza mfalme wake

na Ashkeloni ataachwa pweke.

6 Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

7 Nitaondoa damu vinywani mwao,

chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.

Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,

nao watakuwa viongozi katika Yuda,

naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

8 Lakini nitailinda nyumba yangu

dhidi ya majeshi ya wanyang’anyi.

Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,

kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

9 Shangilia sana, Ee Binti Sayuni!

Piga kelele, Binti Yerusalemu!

Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,

ni mwenye haki naye ana wokovu,

mpole naye amepanda punda,

mwana punda, mtoto wa punda.

10 Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu

na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,

nao upinde wa vita utavunjwa.

Atatangaza amani kwa mataifa.

Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,

na kutoka Mto Eufrati hadi mwisho wa dunia.

11 Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,

nitawaacha huru wafungwa wako

watoke kwenye shimo lisilo na maji.

12 Rudieni ngome yenu, Enyi wafungwa wa tumaini;

hata sasa ninatangaza kwamba

nitawarejesheeni maradufu.

13 Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,

nitamfanya Efraimu mshale wangu.

Nitawainua wana wako, Ee Sayuni,

dhidi ya wana wako, Ee Uyunani,

na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

14 KishaBwanaatawatokea;

mshale wake utamulika

kama umeme wa radi.

BwanaMwenyezi atapiga tarumbeta,

naye atatembea katika tufani za kusini,

15 naBwanaMwenye Nguvu Zote atawalinda.

Wataangamiza na kushinda

kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.

Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;

watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia

kwenye pembe za madhabahu.

16 BwanaMungu wao atawaokoa siku hiyo

kama kundi la watu wake.

Watang’ara katika nchi yake

kama vito vya thamani kwenye taji.

17 Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!

Nafaka itawastawisha vijana wanaume,

nayo divai mpya vijana wanawake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/9-08089358769e121f8d7a1cfb11bd5758.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × three =