Zekaria 2

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia

1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!

2 Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?”

Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”

3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye

4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo.

5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asemaBwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’

6 “Njoni! Njoni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asemaBwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asemaBwana.

7 “Njoo, Ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!”

8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka wewe nyara, kwa kuwa ye yote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake,

9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma.

10 “Piga kelele na ufurahie, Ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asemaBwana.

11 “Mataifa mengi yataunganishwa naBwanasiku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.

12 Bwanaatairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu.

13 Tulieni mbele zaBwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/2-06be10e5a99c4aa4dc8c4b6f42a72993.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nine − 7 =