Zekaria 1

Wito Wa Kumrudia Bwana

1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema:

2 “Bwanaaliwakasirikia sana baba zako wa zamani.

3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asemaBwana.

5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele?

6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?”

“Kisha walitubu na kusema, ‘BwanaMwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ”

Maono Ya Kwanza: Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi

7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa kutawala kwake Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido.

8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.

9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?”

Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.”

10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambaoBwanaamewatuma waende duniani kote.”

11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika waBwana, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.”

12 Kisha malaika waBwanaakasema, “BwanaMwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”

13 Kwa hiyoBwanaakazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.

14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni,

15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’

16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyoshwa Yerusalemu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi naBwanaatamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ”

Maono Ya Pili: Pembe Nne Na Mafundi Wanne

18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne!

19 Nikamwuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”

Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.”

20 KishaBwanaakanionyesha mafundi wanne.

21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”

Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/ZEC/1-820ed10f4b850a2f4b472d51dc147d9d.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven + 15 =