Ayubu 41

1 “Je, waweza kumvua Lewiathanikwa ndoano ya samaki au kufunga ulimi wake kwa kamba? 2 Waweza kupitisha kamba puani mwake au kutoboa taya lake kwa kulabu? 3 Je, ataendelea kukuomba umhurumie? Atasema nawe maneno ya upole? 4 Je, atafanya agano nawe ili umtwae awe mtumishi wako maisha yake yote? 5 Je, utamfuga na kumfanya rafiki […]

Ayubu 42

Ayubu Anamjibu Bwana 1 Ndipo Ayubu akamjibuBwana: 2 “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote, wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika. 3 Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’ Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi, mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua. 4 “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena; nitakuuliza swali, nawe yakupasa […]