Ayubu 21

Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa 1 Ndipo Ayubu akajibu: 2 “Yasikilizeni maneno yangu kwa makini, hii na iwe faraja mnayonipa mimi. 3 Nivumilieni ninapozungumza, nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki. 4 “Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira? 5 Niangalieni mkastaajabu; mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu. 6 Ninapowaza juu […]

Ayubu 22

Elifazi Anasema: Uovu Wa Ayubu Ni Mkubwa 1 Ndipo Elifazi, Mtemani akajibu: 2 “Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu? Je, hata mtu mwenye hekima aweza kujifaidia mwenyewe? 3 Je, Mwenyezi angefurahia nini kama ungekuwa mwadilifu? Au je, yeye angepata faida gani ikiwa njia zako zingekuwa kamilifu? 4 “Je, ni kwa ajili ya utaua […]

Ayubu 23

Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu 1 Ndipo Ayubu akajibu: 2 “Hata leo malalamiko yangu ni uchungu, mkono wake ni mzito juu yangu pamoja na kulia kwangu kwa uchungu. 3 Laiti ningefahamu mahali pa kumwona, laiti ningeweza kwenda mahali akaapo! 4 Ningeliweka shauri langu mbele zake na kukijaza kinywa changu na hoja. 5 Ningejua kwamba […]

Ayubu 24

Ayubu Analalamikia Jeuri Duniani 1 “Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? 2 Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyang’anya kwa nguvu. 3 Huwanyang’anya yatima punda wao na kumchukua rehani fahali wa mjane. 4 Humsukuma mhitaji kutoka katika njia na […]

Ayubu 25

Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu? 1 Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu: 2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu, yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. 3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? 4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? 5 […]

Ayubu 26

Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki 1 Kisha Ayubu akajibu: 2 “Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo! Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu! 3 Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima? Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha! 4 Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo? Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako? 5 […]

Ayubu 27

Ayubu Anadumisha Uadilifu wake 1 Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: 2 “Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu, Mwenyezi ambaye amenifanya nionje uchungu wa nafsi, 3 kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu, nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu, 4 midomo yangu haitanena uovu, wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu. 5 Sitakubaliana […]

Ayubu 28

Mapumziko: Imani Inakopatikana 1 “Kuna machimbo ya fedha na mahali dhahabu isafishwapo. 2 Chuma hupatikana ardhini, nayo shaba huyeyushwa kutoka kwenye mawe ya madini. 3 Mwanadamu hukomesha giza, huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali, kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini katika giza jeusi sana. 4 Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu, mahali paliposahaulika […]

Ayubu 29

Ayubu Anamaliza Utetezi wake 1 Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema: 2 “Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita, zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda, 3 wakati taa yake iliponiangazia juu ya kichwa changu na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza! 4 Aha! Katika siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu, wakati urafiki wa Mungu wa […]

Ayubu 30

1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuliko mimi wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. 2 Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? 3 Kukonda kwao kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizungukazunguka usiku katika nchi kame […]