Ayubu 31

1 “Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani. 2 Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni nini kutoka kwa Mungu juu, nao urithi wake ni nini kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu! 3 Je, si uharibifu kwa watu waovu, maangamizi kwa wale watendao mabaya? 4 Je, yeye hazioni njia zangu na kuihesabu kila […]

Ayubu 32

Elihu Awakemea Rafiki Za Ayubu 1 Basi watu hawa watatu wakaacha kumjibu Ayubu, kwa kuwa alikuwa mwadilifu machoni pake mwenyewe. 2 Lakini Elihu mwana wa Barakeli, wa kabila la Buzi wa jamaa ya Ramu, akamkasirikia sana Ayubu, kwa sababu amejihesabia haki mwenyewe badala ya Mungu. 3 Pia aliwakasirikia hao rafiki watatu wa Ayubu, kwa sababu […]

Ayubu 33

Elihu Anamkemea Ayubu 1 “Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu, zingatia kila kitu nitakachosema. 2 Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. 3 Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu, midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. 4 Roho wa Mungu ameniumba, pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. 5 Unijibu basi, kama […]

Ayubu 34

Elihu Anatangaza Haki Ya Mungu 1 Kisha Elihu akasema: 2 “Sikieni maneno yangu, enyi watu wenye hekima; nisikilizeni mimi, ninyi watu wenye maarifa. 3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula. 4 Tujichagulie wenyewe yaliyo sawa, nasi tujifunze pamoja yaliyo mema. 5 “Ayubu anasema, ‘Mimi sina hatia, lakini Mungu ameninyima haki yangu. […]

Ayubu 35

Elihu Analaumu Mtu Kujiona Kuwa Mwenye Haki 1 Ndipo Elihu akasema: 2 “Je, unadhani hili ni haki? Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’ 3 Bado unamwuliza, ‘Ni faida gani nimepata na nimefaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’ 4 “Ningependa nikujibu wewe pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe. 5 Tazama juu mbinguni ukaone, yaangalie mawingu […]

Ayubu 36

Elihu Atukuza Wema Wa Mungu 1 Elihu akaendelea na kusema: 2 “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. 3 Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu. 4 Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; yeye aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na […]

Ayubu 37

1 “Kwa hili moyo wangu unatetemeka, nao unaruka kutoka mahali pake. 2 Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake, sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake. 3 Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote na kuupeleka hata miisho ya dunia. 4 Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake, Mungu hunguruma kwa sauti yake ya […]

Ayubu 38

SEHEMU YA NNE: MUNGU ANAZUNGUMZA Bwana Anamjibu Ayubu 1 KishaBwanaakamjibu Ayubu kutoka katika upepo wa kisulisuli. Akasema: 2 “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? 3 Jikaze kama mwanaume, nami nitakuuliza swali, nawe unijibu. 4 “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu. 5 Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? […]

Ayubu 39

1 “Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa? Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake? 2 Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo? Je, unajua majira yao ya kuzaa? 3 Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao, utungu wa kuzaa unakoma. 4 Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani, huenda zao wala […]

Ayubu 40

1 Bwanaakamwambia Ayubu: 2 “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha? Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.” 3 Ndipo Ayubu akamjibuBwana: 4 “Mimi sistahili kabisa, ninawezaje kukujibu wewe? Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu. 5 Nimesema mara moja, lakini sina jibu; naam, nimesema mara mbili, lakini sitasema tena.” 6 NdipoBwanaakasema na Ayubu kutoka katika upepo […]