Ezekieli 41

1 Kisha yule mtu akanileta katika sehemu ya nje ya patakatifu naye akaipima miimo, upana wake ulikuwa dhiraa sitakila upande. 2 Ingilio lilikuwa la upana wa dhiraa kumi na kuta zilizojitokeza kila upande zilikuwa na upana wa dhiraa tano. Pia akapima sehemu ya nje ya patakatifu, nayo ilikuwa na urefu wa dhiraa arobainina upana wa […]

Ezekieli 42

Vyumba Vya Makuhani 1 Ndipo yule mtu akaniongoza kuelekea kaskazini mpaka kwenye ua wa nje na kunileta mpaka kwenye vyumba vinavyoelekeana na ua wa Hekalu na kuelekeana na ukuta wa nje upande wa kaskazini. 2 Jengo ambalo mlango wake ulielekea kaskazini lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini. 3 Mbele […]

Ezekieli 43

Utukufu Warudi Hekaluni 1 Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 2 nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikang’aa kwa utukufu wake. 3 Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja […]

Ezekieli 44

Mkuu, Walawi, Makuhani 1 Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali Patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. 2 Bwanaakaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu ye yote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababuBwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili. 3 […]

Ezekieli 45

Mgawanyo Wa Nchi 1 “ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwaBwanakuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000upana wake dhiraa 20,000, eneo hili lote litakuwa takatifu. 2 Katika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. 3 Katika […]

Ezekieli 46

Sheria Nyingine Mbalimbali 1 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa. 2 Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa […]

Ezekieli 47

Mto Kutoka Hekaluni 1 Yule mtu akanirudisha mpaka kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki). Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kusini wa Hekalu, kusini mwa madhabahu. 2 Ndipo akanitoa nje kupitia lango la kaskazini na […]

Ezekieli 48

Mgawanyo Wa Nchi 1 “Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enoni hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi. 2 “Asheri […]