Ezra 1

Koreshi Asaidia Watu Kurudi Kutoka Uhamishoni

1 Katika mwaka wa kwanza wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kutimiza neno laBwanalililosemwa na Yeremia,Bwanaaliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote na kuliweka katika maandishi:

2 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:

“ ‘Bwana, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za duniani na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda.

3 Ye yote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha apande kwenda Yerusalemu katika Yuda na kujenga Hekalu laBwana, Mungu wa Israeli, Mungu aliyeko huko Yerusalemu.

4 Nao watu wa mahali po pote wale walionusurika wanapoishi sasa, watu hao wampe fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, mbali na sadaka za hiari kwa ajili ya Hekalu la Mungu huko Yerusalemu.’ ”

5 Kisha viongozi wa jamaa ya Yuda na Benyamini na makuhani na Walawi kila mmoja ambaye moyo wake ulisukumwa na Mungu, akajiandaa kupanda ili kuijenga nyumba yaBwanahuko Yerusalemu.

6 Majirani zao wote wakawasaidia vyombo vya fedha na dhahabu, pamoja na vifaa na mifugo, pia na zawadi za thamani, pamoja na sadaka zote za hiari.

7 Zaidi ya hayo, Mfalme Koreshi akavitoa vyombo vilivyokuwa mali ya Hekalu laBwana, ambavyo Nebukadneza alikuwa amevichukua kutoka Yerusalemu na kuviweka katika hekalua la mungu wake.

8 Koreshi mfalme wa Uajemi akavitoa kwa mkono wa Mithredathi mtunza hazina, aliyevihesabu mbele ya Sheshbaza mkuu wa Yuda.

9 Hii ilikuwa ndio orodha ya vifaa:

masinia ya dhahabu yalikuwa 30
masinia ya fedha yalikuwa 1,000
vyetezo vya fedha vilikuwa 29
10 mabakuli ya dhahabu yalikuwa 30
mabakuli ya fedha yanayofanana yalikuwa 410
vifaa vingine vilikuwa 1,000.

11 Kwa ujumla, kulikuweko na vyombo 5,400 vya dhahabu na vya fedha. Sheshbaza akavileta hivi vyote wakati watu walipotoka uhamishoni Babeli kwenda Yerusalemu.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/EZR/1-0dc481afe6e1fa96d3f5bae426bc45ec.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − seventeen =