Mwanzo 11

Mnara Wa Babeli 1 Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 2 Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinarinao wakaishi huko. 3 Wakasemezana wao kwa wao, “Njoni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo […]

Mwanzo 12

Wito Wa Abramu 1 Bwanaakawa amemwambia Abramu, “Ondoka katika nchi yako, waache watu wako na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha. 2 “Mimi nitakufanya taifa kubwa na nitakubariki, Nitalikuza jina lako, nawe utakuwa baraka. 3 Nitawabariki wale wanaokubariki, na ye yote akulaaniye nitamlaani; na kupitia kwako mataifa yote duniani yatabarikiwa.” 4 Hivyo Abramu […]

Mwanzo 13

Abramu Na Loti Watengana 1 Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Loti akaenda pamoja naye. 2 Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu. 3 Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati […]

Mwanzo 14

Abramu Amwokoa Loti 1 Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu 2 kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). 3 Hawa […]

Mwanzo 15

Agano La Mungu Na Abramu 1 Baada ya jambo hili, neno laBwanalikamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” 2 Lakini Abramu akasema, “EeBwanaMwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 3 Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba […]

Mwanzo 16

Hagari Na Ishmaeli 1 Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari, 2 hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwanaamenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. 3 Hivyo baada ya Abramu kuishi […]

Mwanzo 17

Agano La Tohara 1 Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa,Bwanaakamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi; enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. 2 Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.” 3 Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 4 “Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa […]

Mwanzo 18

Wageni Watatu 1 Bwanaakamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. 2 Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi. 3 Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite […]

Mwanzo 19

Kuangamizwa Kwa Sodoma Na Gomora 1 Malaika wale wawili wakafika Sodoma wakati wa jioni, naye Loti alikuwa ameketi kwenye lango la mji. Wakati alipowaona, aliondoka kwenda kuwalaki na kuwasujudia hadi chini. 2 Akasema, “Bwana zangu, tafadhali karibuni kwenye nyumba ya mtumishi wenu. Mnaweza kunawa miguu na kulala hapa kisha asubuhi na mapema mwendelee na safari […]

Mwanzo 20

Abrahamu Na Abimeleki 1 Basi Abrahamu akaendelea mbele kutoka huko hadi nchi ya Negebu na akaishi kati ya Kadeshi na Shuri. Kwa muda mfupi alikaa Gerari kama mgeni, 2 huko Abrahamu akasema kuhusu Sara mkewe, “Huyu ni dada yangu.” Kisha Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma Sara aletwe, naye akamchukua. 3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika […]