Zaburi 131

Maombi Ya Kumtegemea Mungu Kwa Unyenyekevu (Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi.) 1 Moyo wangu hauna kiburi, EeBwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu. 2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani […]

Zaburi 132

Maskani Ya Mungu Ya Milele Katika Sayuni (Wimbo Wa Kwenda Juu) 1 EeBwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. 2 Aliapa kiapo kwaBwana na akaweka nadhiri kwa yeye Mwenye Nguvu wa Yakobo: 3 “Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: 4 sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, 5 mpaka nitakapompatiaBwanamahali, makao kwa […]

Zaburi 133

Sifa Za Pendo La Undugu (Wimbo Wa Kwenda Juu. Wa Daudi) 1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! 2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. 3 Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu […]

Zaburi 134

Wito Wa Kumsifu Mungu (Wimbo Wa Kwenda Juu) 1 MsifuniBwana, ninyi nyote watumishi waBwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba yaBwana. 2 Inueni mikono yenu katika mahali patakatifu na mumsifuBwana. 3 NayeBwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni. —https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/PSA/134-0ab0f077880d8b738f1866dcc6bb3977.mp3?version_id=1627—

Zaburi 135

Wimbo Wa Sifa Kwa Mungu 1 MsifuniBwana. Lisifuni jina laBwana, msifuni, enyi watumishi waBwana, 2 ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba yaBwana, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. 3 MsifuniBwana, kwa kuwaBwanani mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. 4 Kwa maanaBwanaamemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani. […]

Zaburi 136

Wimbo Wa Kumshukuru Mungu 1 MshukuruniBwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. 2 Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. 4 Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. 5 Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. 6 […]

Zaburi 137

Maombolezo Ya Israeli Uhamishoni 1 Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaomboleza tulipokumbuka Sayuni. 2 Kwenye miti ya huko tulitundika vinubi vyetu, 3 kwa maana huko hao waliotuteka walitaka tuwaimbie nyimbo, watesi wetu walidai nyimbo za furaha; walisema, “Tuimbieni wimbo mmoja kati ya nyimbo za Sayuni!” 4 Tutaimbaje nyimbo zaBwana, tukiwa katika nchi ya kigeni? […]

Zaburi 138

Maombi Ya Shukrani (Zaburi Ya Daudi) 1 Nitakusifu wewe, EeBwana, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. 2 Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote. 3 Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na […]

Zaburi 139

Mungu Asiyeweza Kukwepwa (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, umenichunguza na kunijua. 2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. 3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. 4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, EeBwana. 5 Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. […]

Zaburi 140

Kuomba Ulinzi Wa Mungu (Kwa Mwimbishaji: Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri, 2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao na kuchochea vita siku zote. 3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka imo midomoni mwao. 4 EeBwana, niepushe na mikono ya waovu; […]