Zaburi 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu (Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita. 2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni. 3 EeBwana, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu. 4 Usiuache moyo wangu […]

Zaburi 142

Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Watesi (Utenzi Wa Daudi Alipokuwa Pangoni. Maombi) 1 NamliliaBwanakwa sauti kubwa, nainua sauti yangu kwaBwanaanihurumie. 2 Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu. 3 Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameweka mtego kwa ajili yangu. 4 Tazama kuume […]

Zaburi 143

Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Adui (Zaburi Ya Daudi) 1 EeBwana, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie. 2 Usimhukumu mtumishi wako, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi mwenye haki mbele zako. 3 Adui hunifuatilia, hunipondaponda chini; hunifanya niishi gizani kama wale waliokufa zamani. 4 Kwa hiyo roho yangu […]

Zaburi 144

Mfalme Amshukuru Mungu Kwa Ushindi (Zaburi Ya Daudi) 1 Sifa ni kwaBwanaMwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, vidole vyangu kupigana. 2 Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. 3 EeBwana, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie? […]

Zaburi 145

Wimbo Wa Kusifu Ukuu Na Wema Wa Mungu (Wimbo Wa Sifa. Wa Daudi) 1 Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele. 2 Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele. 3 Bwanani mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki. 4 Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia […]

Zaburi 146

Kumsifu Mungu Mwokozi 1 MsifuniBwana! Ee nafsi yangu, umsifuBwana, 2 NitamsifuBwanamaisha yangu yote; nitamwimbia Mungu wangu sifa wakati wote niishipo. 3 Usiweke tumaini lako kwa wakuu, kwa wanadamu ambao hufa, ambao hawawezi kuokoa. 4 Roho yao itokapo hurudi mavumbini, siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma. 5 Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada […]

Zaburi 147

Kumsifu Mungu Mwenye Nguvu Zote 1 MsifuniBwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye! 2 Bwanahujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni. 3 Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao. 4 Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake. 5 Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu […]

Zaburi 148

Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu 1 MsifuniBwana. MsifuniBwanakutoka mbinguni, msifuni juu vileleni. 2 Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni. 3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zing’aazo. 4 Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana na ninyi maji juu ya anga. 5 Vilisifu […]

Zaburi 149

Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake 1 MsifuniBwana. MwimbieniBwanawimbo mpya, sifa zake katika kusanyiko la watakatifu. 2 Israeli na washangilie katika Muumba wao, watu wa Sayuni na wafurahi katika mfalme wao. 3 Na walisifu jina lake kwa kucheza na wampigie muziki kwa matari na kinubi. 4 Kwa maanaBwanaanapendezwa na watu wake, anawavika wanyenyekevu taji […]

Zaburi 150

Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake 1 MsifuniBwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze, 4 Msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, […]