Mwanzo 22

Kujua Uthabiti Wa Abrahamu

1 Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”

Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”

2 Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia.

4 Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali.

5 Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.”

6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja,

7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”

Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”

Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”

8 Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni.

10 Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe.

11 Lakini malaika waBwanaakamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lo lote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.

14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire, yaaniBwanaatatupatia. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima waBwanaitapatikana.”

15 Basi malaika waBwanaakamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili,

16 akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asemaBwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee,

17 hakika, nitakubariki na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,

18 na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”

19 Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.

Wana Wa Nahori

20 Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana:

21 Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu),

22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.”

23 Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane.

24 Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/22-82dbfe1a03e13c70a748d1dba50033f8.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 23

Kifo Cha Sara

1 Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba.

2 Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara.

3 Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema,

4 “Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.”

5 Wahiti wakamjibu Abrahamu,

6 “Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.”

7 Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti.

8 Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu

9 ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.”

10 Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji.

11 “La hasha, bwana wangu, nisikilize, nakupa shamba, pia nakupa pango lililomo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu. Uzike maiti wako.”

12 Abrahamu akasujudu tena, mbele ya wenyeji wa nchi,

13 akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.”

14 Efroni akamjibu Abrahamu,

15 “Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha, lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”

16 Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.

17 Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwemo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa,

18 kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji.

19 Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani.

20 Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/23-0efe194da9756d5b560376b94a464b13.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 24

Isaki Na Rebeka

1 Wakati huu Abrahamu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, nayeBwanaalikuwa amembariki katika kila njia.

2 Akamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu,

3 Ninataka uape kwaBwana, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka katika binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao,

4 bali utakwenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaki mwanangu mke.”

5 Yule mtumishi akamwuliza, “Je, kama huyo mwanamke atakataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimpeleke mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?”

6 Abrahamu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko.

7 Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa nyumbani kwa baba yangu na nchi yangu niliyozaliwa na aliyesema nami na akaniahidi kwa kiapo, akisema, ‘Nitawapa watoto wako nchi hii,’ atatuma malaika wake akutangulie ili umpatie mwanangu mke kutoka huko.

8 Kama huyo mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi utafunguliwa kutoka kiapo nilichokuapisha. Ila usimrudishe mwanangu huko.”

9 Basi yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la bwana wake Abrahamu akamwapia kuhusu shauri hili.

10 Ndipo huyo mtumishi akachukua ngamia kumi miongoni mwa ngamia za bwana wake akaondoka, akachukua aina zote za vitu vizuri kutoka kwa bwana wake. Akaelekea Aramu-Naharaimuna kushika njia kwenda mji wa Nahori.

11 Akawapigisha ngamia magoti karibu na kisima cha maji nje ya mji, ilikuwa inaelekea jioni, wakati ambapo wanawake wanakuja kuteka maji.

12 Kisha akaomba, “EeBwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, nipatie ushindi leo, uonyeshe huruma kwa bwana wangu Abrahamu.

13 Tazama, nimesimama karibu na kisima hiki cha maji, nao binti za watu wa mji huu wanakuja kuteka maji.

14 Basi na iwe hivi, nitakapomwambia binti mmojawapo, ‘Tafadhali tua mtungi wako nipate kunywa maji,’ naye akisema, ‘Kunywa, nitawanywesha na ngamia wako pia.’ Basi na awe ndiye uliyemchagua kwa ajili ya mtumishi wako Isaki. Kwa hili nitajua umemhurumia bwana wangu.”

15 Ikawa kabla hajamaliza kuomba, Rebeka akatokea akiwa na mtungi begani mwake. Alikuwa binti wa Bethueli. Bethueli alikuwa mwana wa Milka aliyekuwa mke wa Nahori ndugu wa Abrahamu.

16 Huyu msichana alikuwa mzuri sana wa sura, bikira, ambaye hakuna mtu aliyekuwa amekutana naye kimwili. Alitelemka kisimani, akajaza mtungi wake akapanda juu.

17 Ndipo yule mtumishi akaharakisha kukutana naye akamwambia, “Tafadhali nipe maji kidogo katika mtungi wako.”

18 Yule msichana akasema, “Kunywa, bwana wangu.” Akashusha kwa haraka mtungi mkononi mwake na akampa, akanywa.

19 Baada ya kumpa yule mtumishi yale maji, akamwambia, “Nitateka maji kwa ajili ya ngamia zako pia mpaka wote watosheke.”

20 Akafanya haraka kumimina maji kwenye birika ya kunyweshea wanyama, akakimbia kisimani kuteka maji mengine na akateka ya kuwatosha ngamia wake wote.

21 Pasipo kusema neno, yule mtumishi akamtazama kwa makini aone kamaBwanaameifanikisha safari yake, au la.

22 Ikawa ngamia walipokwisha kunywa wote, yule mtumishi akampa huyo msichana pete ya puani ya dhahabu yenye uzito wa beka mojana bangili mbili za dhahabu zenye uzito wa shekeli kumi.

23 Kisha akamwuliza, “Wewe ni binti wa nani? Tafadhali uniambie, je, kuna nafasi katika nyumba ya baba yako tutakapoweza kulala?”

24 Yule msichana akamjibu, “Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Milka aliyemzalia Nahori.”

25 Akaendelea kusema, “Kwetu kuna majani mengi na malisho, tena kuna nafasi kwa ajili yenu kulala.”

26 Yule mtumishi akasujudu na kumwabuduBwana,

27 akisema, “AtukuzweBwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye hakuondoa wema na uaminifu wake kwa bwana wangu. Mimi nami,Bwanaameniongoza safarini akanifikisha nyumbani kwa jamaa za bwana wangu.”

28 Yule msichana akakimbia akawaeleza watu wa nyumbani mwa mama yake kuhusu mambo haya.

29 Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani, huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani.

30 Mara alipoiona ile pete puani, na bangili mikononi mwa dada yake na kusikia yale maneno Rebeka aliyoambiwa na huyo mtumishi, alimwendea huyo mtumishi, akamkuta amesimama karibu na ngamia wake pale karibu na kisima.

31 Akamwambia, “Karibu nyumbani wewe uliyebarikiwa naBwana, kwa nini unasimama huko nje? Mimi nimekuandalia nyumba na mahali kwa ajili ya ngamia.”

32 Hivyo yule mtumishi akaenda nyumbani, mizigo ikaondolewa juu ya ngamia. Majani na malisho yakaletwa kwa ajili ya ngamia na maji kwa ajili yake na watu wake ili kunawa miguu.

33 Ndipo chakula kikaandaliwa kwa ajili yake, lakini akasema, “Sitakula mpaka niwe nimewaambia yale niliyo nayo ya kusema.”

Labani akasema, “Basi tuambie.”

34 Hivyo akasema, “Mimi ni mtumishi wa Abrahamu.

35 Bwanaamembariki sana bwana wangu, amekuwa tajiri. Amempa kondoo na ng’ombe, fedha na dhahabu, watumishi wa kiume na wa kike, ngamia na punda.

36 Sara mkewe bwana wangu amemzalia mwana katika uzee wake, naye amempa kila kitu alichokuwa nacho.

37 Naye bwana wangu ameniapisha na akasema, ‘Kamwe usimtwalie mwanangu mke katika binti za Wakanaani, ambao ninaishi katika nchi yao,

38 ila uende mpaka kwa jamaa ya baba yangu na ukoo wangu mwenyewe, ukamtwalie mwanangu mke huko.’

39 “Kisha nikamwuliza bwana wangu, ‘Je, kama huyo mwanamke hatakubali kurudi nami?’

40 “Akanijibu, ‘Bwanaambaye nimetembea mbele zake, atatuma malaika wake pamoja nawe, na kuifanikisha safari yako, ili uweze kupata mke kwa ajili ya mwanangu katika ukoo wangu na kutoka katika jamaa ya baba yangu.

41 Kisha, utakapokwenda kwenye ukoo wangu, utakuwa umefunguliwa kutoka katika kiapo changu hata kama wakikataa kukupa huyo binti, utakuwa umefunguliwa kutoka kiapo changu.’

42 “Nilipokuja kisimani leo nilisema, ‘EeBwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ikikupendeza, naomba uifanikishe safari niliyoijia.

43 Tazama, ninasimama kando ya kisima hiki, kama mwanamwali akija kuteka maji nami nikimwambia, tafadhali niruhusu ninywe maji kidogo kutoka kwenye mtungi wako,

44 naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambayeBwanaamemchagulia mwana wa bwana wangu.’

45 “Kabla sijamaliza kuomba moyoni mwangu, Rebeka akatokea, amebeba mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka maji, nami nikamwambia, ‘Tafadhali unipe maji ninywe.’

46 “Akafanya haraka kushusha mtungi wake begani na kusema, ‘Kunywa na nitawanywesha ngamia wako pia,’ basi nikanywa, akawanywesha na ngamia pia.

47 “Nikamwuliza, ‘Wewe ni binti wa nani?’

“Akasema, ‘Mimi ni binti wa Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia.’

“Ndipo nilipotia pete puani mwake na bangili mikononi mwake,

48 nikasujudu na nikamwabuduBwana. NikamtukuzaBwana, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake.

49 Ikiwa mtaonyesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie, la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.”

50 Labani na Bethueli wakajibu, “Jambo hili limetoka kwaBwana, hatuwezi kukuambia jambo lo lote baya au jema.

51 Rebeka yuko hapa, mchukue na uende, awe mke wa mwana wa bwana wako, sawasawa naBwanaalivyoongoza.”

52 Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu mpaka nchi mbele zaBwana.

53 Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha pamoja na mavazi, akampa Rebeka, pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye.

54 Kisha yeye na wale watu waliokuwa pamoja naye wakala, wakanywa na kulala pale pale.

Walipoamka asubuhi, yule mtumishi, akasema, “Nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”

55 Lakini ndugu yake Rebeka pamoja na mama yake wakajibu, “Acha binti akae kwetu siku kumi au zaidi, ndipo mwondoke.”

56 Lakini yule mtumishi akawaambia, “Msinicheleweshe, kwa kuwaBwanaamefanikisha safari yangu, nipeni ruhusa nirudi kwa bwana wangu.”

57 Ndipo wakasema, “Acha tumwite huyo binti tumwulize, tusikie atakavyosema.”

58 Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumwuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?”

Akasema, “Nitakwenda.”

59 Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake.

60 Wakambariki Rebeka, wakamwambia,

“Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu,

mara elfu nyingi,

nao wazao wako wamiliki

malango ya adui zao.”

61 Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka.

62 Basi Isaki alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa anaishi nchi ya Negebu.

63 Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja.

64 Rebeka pia akainua macho akamwona Isaki. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake

65 na akamwuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule aliye kule shambani anayekuja kutulaki?”

Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.

66 Kisha yule mtumishi akamweleza Isaki mambo yote aliyoyatenda.

67 Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/24-74c526e8f7d99d61c83521a078b9a7ac.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 25

Kifo Cha Abrahamu

1 Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura.

2 Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

3 Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi.

4 Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura.

5 Abrahamu akamwachia Isaki kila kitu alichokuwa nacho.

6 Lakini alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki.

7 Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175.

8 Ndipo Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa mwenye umri mzuri, akiwa mzee ameshiba siku, akakusanywa pamoja na watu wake.

9 Watoto wake Isaki na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti,

10 Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara.

11 Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu akambariki mwanawe Isaki, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi.

Wana Wa Ishmaeli

12 Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu.

13 Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli Mibsamu,

14 Mishma, Duma, Masa,

15 Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema.

16 Hawa walikuwa wana wa Ishmaeli na haya ni majina ya viongozi wa makabila kumi na mawili kulingana na makao yao na kambi zao.

17 Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake.

18 Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, unapoelekea Ashuri. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote.

Yakobo Na Esau

19 Hivi ndivyo vizazi vya Isaki mwana wa Abrahamu.

Abrahamu akamzaa Isaki,

20 Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu.

21 Isaki akamwombaBwanakwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa.Bwanaakajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.

22 Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumwulizaBwana.

23 Bwanaakamjibu,

“Mataifa mawili yamo tumboni mwako,

na mataifa hayo mawili

kutoka ndani yako watatenganishwa,

mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine,

na mkubwa atamtumikia mdogo.”

24 Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake.

25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele, wakamwita jina lake Esau.

26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ulikuwa umemshika Esau kisigino, akaitwa jina lake Yakobo. Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.

27 Watoto wakakua, Esau alikuwa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, wakati Yakobo alikuwa mtu mkimya, mwenye kukaa nyumbani.

28 Isaki, ambaye alikuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.

29 Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali.

30 Akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)

31 Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”

32 Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu ya kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?”

33 Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya kuzaliwa.

34 Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake.

Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/25-f1f72cece546ea2e9991c4d15a030565.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 26

Isaki Na Abimeleki

1 Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari.

2 Bwanaakamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia.

3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.

4 Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa,

5 kwa sababu Abrahamu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.”

6 Hivyo Isaki akaishi huko Gerari.

7 Watu wa mahali pale walipomwuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumwua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”

8 Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake.

9 Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ”

Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.”

10 Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu ye yote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.”

11 Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Ye yote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.”

12 Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka uo huo, akavuna mara mia, kwa sababuBwanaalimbariki.

13 Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana.

14 Akawa na kondoo, ng’ombe na watumishi wengi sana kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu.

15 Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia wakavijaza udongo.

16 Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.”

17 Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko.

18 Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.

19 Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi.

20 Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,kwa sababu waligombana naye.

21 Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.

22 Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna ye yote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,akisema, “SasaBwanaametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”

23 Kutoka pale akaenda Beer-Sheba.

24 Usiku uleBwanaakamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.”

25 Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina laBwana. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima.

26 Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake.

27 Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?”

28 Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwaBwanaalikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe

29 kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa naBwana.’ ”

30 Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa.

31 Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.

32 Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!”

33 Naye akakiita Shiba,mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba.

34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti.

35 Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/26-594434aee43f6597886a8ffca93a4760.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 27

Yakobo Anaipata Baraka Ya Isaki

1 Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.”

Akajibu, “Mimi hapa.”

2 Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu.

3 Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upindi, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu.

4 Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.”

5 Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta,

6 Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau,

7 ‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele zaBwanakabla sijafa.’

8 Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia:

9 Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyotaka.

10 Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.”

11 Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Lakini ndugu yangu Esau ana nywele mwilini, mimi nina ngozi nyororo.

12 Itakuwaje kama baba yangu akinigusa? Itaonekana kwake kama niliyemfanyia ujanja na kuleta laana juu yangu badala ya baraka.”

13 Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia, nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.”

14 Kwa hiyo alikwenda akawaleta, akampa mama yake, akaandaa chakula kitamu, kama vile alivyotaka baba yake.

15 Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.

16 Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi.

17 Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka.

18 Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.”

Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”

19 Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

20 Isaki akamwuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?”

Akajibu, “BwanaMungu wako amenifanikisha.”

21 Kisha Isaki akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.”

22 Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaki, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.”

23 Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki.

24 Akamwuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?”

Akajibu, “Mimi ndiye.”

25 Kisha akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nipate kukubariki.”

Yakobo akamletea naye akala, akamletea na divai akanywa.

26 Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.”

27 Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema,

“Aha, harufu ya mwanangu

ni kama harufu ya shamba

ambaloBwanaamelibariki.

28 Mungu na akupe umande kutoka mbinguni

na utajiri wa duniani:

wingi wa nafaka na divai mpya.

29 Mataifa na yakutumikie

na mataifa yakusujudie.

Uwe bwana juu ya ndugu zako,

na wana wa mama yako wakusujudie.

Walaaniwe wale wakulaanio,

nao wale wakubarikio wabarikiwe.”

30 Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.

31 Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”

32 Isaki baba yake akamwuliza, “Wewe ni nani?”

Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.”

33 Isaki akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!”

34 Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”

35 Lakini akasema, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako.”

36 Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?”

37 Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?”

38 Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.

39 Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia,

“Makao yako yatakuwa

mbali na utajiri wa dunia,

mbali na umande wa mbinguni juu.

40 Utaishi kwa upanga,

nawe utamtumikia ndugu yako,

lakini wakati utakapokuwa umejikomboa,

utatupa nira yake

kutoka shingoni mwako.”

Yakobo Anakimbilia Kwa Labani

41 Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia, ndipo nitamwua ndugu yangu Yakobo.”

42 Rebeka alipokwisha kuambiwa yale aliyoyasema Esau mwanawe mkubwa, alimwita Yakobo mwanawe mdogo, akamwambia, “Ndugu yako Esau anajifariji kwa wazo la kukuua.

43 Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani.

44 Ukae naye kwa muda mpaka ghadhabu ya ndugu yako itulie.

45 Wakati ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze wote wawili kwa siku moja?”

46 Kisha Rebeka akamwambia Isaki, “Nimechukia kuishi kwa sababu ya hawa wanawake wa Kihiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake wa Kihiti kama hawa, sitakuwa na faida kuendelea kuishi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/27-177403a3692550942c4595eb42391977.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 28

1 Basi Isaki akamwita Yakobo, akambariki na akamwamuru, akisema, “Usioe mwanamke wa Kikanaani.

2 Nenda mara moja mpaka Padan-Aramu, kwenye nyumba ya Bethueli baba wa mama yako. Uchukue mke kati ya binti za Labani ambaye ni ndugu wa mama yako.

3 Mungu Mwenyezina akubariki uwe na uzao uongezeke idadi yako upate kuwa jamii kubwa ya watu.

4 Na akupe wewe na uzao wako baraka aliyopewa Abrahamu, upate kumiliki nchi unayoishi sasa kama mgeni, nchi ambayo Mungu alimpa Abrahamu.”

5 Kisha Isaki akamuaga Yakobo, naye akaenda Padan-Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, ndugu wa Rebeka, aliyekuwa mama wa Yakobo na Esau.

6 Sasa Esau akajua kuwa Isaki amembariki Yakobo na kumtuma kwenda Padan-Aramu ili achukue mke huko na kwamba alipombariki alimwamuru akisema, “Usioe mke katika binti za Wakanaani,”

7 tena kwamba Yakobo amewatii baba yake na mama yake naye amekwenda Padan-Aramu.

8 Esau akatambua jinsi ambavyo baba yake Isaki anavyowachukia binti za Wakanaani,

9 ndipo akaenda kwa Ishmaeli akamwoa Mahalati, ndugu wa Nebayothi na binti wa Ishmaeli mwana wa Abrahamu, kuongezea wale wake wengine aliokuwa nao.

Ndoto Ya Yakobo Huko Betheli

10 Yakobo akatoka Beer-Sheba kwenda Harani.

11 Alipofika mahali fulani, akalala hapo kwa sababu jua lilikuwa limetua. Akachukua jiwe moja la mahali pale, akaliweka chini ya kichwa chake akajinyoosha akalala usingizi.

12 Akaota ndoto ambayo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni na malaika wa Mungu wakawa wakipanda na kushuka juu yake.

13 Juu yake alisimamaBwana, akasema, “Mimi niBwana, Mungu wa baba yako Abrahamu na Mungu wa Isaki. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.

14 Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako mataifa yote ya duniani yatabarikiwa.

15 Niko pamoja nawe nami nitakulinda kila uendako na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha mpaka nitakapofanya hayo niliyokuahidi.”

16 Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “HakikaBwanayuko mahali hapa, wala mimi sikujua.”

17 Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.”

18 Asubuhi yake na mapema, Yakobo akalichukua lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.

19 Mahali pale akapaita Betheli, ingawa mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.

20 Kisha Yakobo akaweka nadhiri, akisema, “Kama Mungu akiwa pamoja nami na kunilinda katika safari niendayo, akinipa chakula nile na nguo nivae

21 na nirudi salama nyumbani kwa baba yangu, hapo ndipoBwanaatakuwa Mungu wangu,

22 nalo jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu na katika yote utakayonipa nitakutolea wewe sehemu ya kumi.”

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/28-195626fd5de30f2cdedc043f4e7e178f.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 29

Yakobo Awasili Padan-Aramu

1 Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika kwenye nchi za mataifa ya mashariki.

2 Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho kwa sababu walikuwa wanakunywa maji kutoka kwenye kisimani hicho. Jiwe lililokuwa mdomoni mwa kisima lilikuwa kubwa.

3 Wakati kondoo wanapokuwa wamekusanyika hapo, wachungaji huvingirisha jiwe hilo kutoka kwenye mdomo wa kisima na kunywesha kondoo. Kisha hulirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.

4 Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?”

Wakamjibu, “Tumetoka Harani.”

5 Aliwaambia, “Je, mnamjua Labani, mjukuu wa Nahori?”

Wakamjibu, “Ndiyo, tunamfahamu.”

6 Kisha Yakobo akawauliza, “Je, yeye ni mzima?”

Wakasema, “Ndiyo, ni mzima, na hapa yuaja Raheli binti yake akiwa na kondoo.”

7 Akasema, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya kondoo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”

8 Walijibu, “Haiwezekani, mpaka kondoo wote wakusanyike na jiwe liwe limevingirishwa kutoka mdomo wa kisima. Ndipo tutanywesha kondoo.”

9 Alipokuwa akizungumza nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa baba yake, kwa maana alikuwa mchunga kondoo.

10 Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake.

11 Kisha Yakobo akambusu Raheli na akaanza kulia kwa sauti.

12 Alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake.

13 Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote.

14 Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni nyama yangu na damu yangu mwenyewe.”

Yakobo Awaoa Lea Na Raheli

Baada ya Yakobo kukaa kwa Labani mwezi mzima,

15 Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”

16 Labani alikuwa na binti wawili, binti mkubwa aliitwa Lea na binti mdogo aliitwa Raheli.

17 Lea alikuwa na macho dhaifu, lakini Raheli alikuwa na umbo la kupendeza na mzuri wa sura.

18 Yakobo akampenda Raheli, akamwambia Labani, “Nitakutumikia kwa miaka saba kwa ajili ya kumpata Raheli binti yako mdogo.”

19 Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine ye yote. Kaa pamoja na mimi hapa.”

20 Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli.

21 Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka nikutane naye kimwili.”

22 Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu.

23 Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili.

24 Naye Labani akamtoa Zilpa mtumishi wake wa kike kuwa mtumishi wa binti yake.

25 Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, Sivyo? Kwa nini umenidanganya?”

26 Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa.

27 Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.”

28 Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.

29 Labani akamtoa Bilha mtumishi wake wa kike kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake.

30 Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli zaidi kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba.

Wana Wa Yakobo

31 Bwanaalipoona kwamba Lea hapendwi, akampa watoto, lakini Raheli alikuwa tasa.

32 Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni, kwa maana alisema, “Ni kwa sababuBwanaameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”

33 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababuBwanaalisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.

34 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.

35 Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifuBwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/29-a118ef4ca1b24e58f29da74250466b09.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 30

1 Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!”

2 Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?”

3 Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”

4 Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili,

5 akapata mimba, naye akamzalia mwana.

6 Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipatia haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.

7 Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa pili.

8 Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.

9 Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa naye akampa Yakobo awe mke wake.

10 Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana.

11 Ndipo Lea akasema, “Hii ni bahati nzuri iliyoje!” Kwa hiyo akamwita Gadi.

12 Mtumishi wa kike wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili.

13 Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.

14 Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”

15 Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kumtwaa mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?”

Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.”

16 Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule.

17 Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano.

18 Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.

19 Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita.

20 Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.

21 Baadaye akamzaa mtoto wa kike akamwita Dina.

22 Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake.

23 Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

24 Akamwita Yosefuna kusema, “Bwanana anipe mwana mwingine.”

Makundi Ya Yakobo Yaongezeka

25 Baada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu.

26 Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.”

27 Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwambaBwanaamenibariki kwa sababu yako.”

28 Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.”

29 Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi ambavyo nimekutumikia na jinsi ambavyo wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu.

30 Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, nayeBwanaamekubariki po pote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?”

31 Labani akamwuliza, “Nikupe nini?”

Yakobo akamjibu, “Usinipe cho chote lakini kama utanifanyia jambo hili moja, nitaendelea kuchunga na kuyaangalia makundi yako.

32 Niruhusu nipite katika makundi yako yote leo niondoe humo kila kondoo mwenye mabakabaka au madoadoa, kila mwana-kondoo mweusi na kila mbuzi mwenye madoadoa au mabakabaka. Hawa watakuwa ujira wangu.

33 Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi ye yote wangu ambaye hana mabakabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.”

34 Labani akasema, “Ninakubali na iwe kama ulivyosema.”

35 Siku ile ile Yakobo akawaondoa beberu wote waliokuwa na mistari au madoadoa na mbuzi wake wote waliokuwa na mistari au madoadoa (wote waliokuwa na alama nyeupe juu yao) na wana-kondoo weusi wote, akawaweka chini ya uangalizi wa wanawe.

36 Kisha Labani akamwacha Yakobo kwa mwendo wa safari ya siku tatu kati yake na Yakobo, wakati Yakobo akiendelea kuchunga lile kundi la Labani lililobaki.

37 Hata hivyo, Yakobo, akachukua fito mbichi zilizokatwa wakati huo huo za miti ya mlubna, mlozi na mwaramoni akazibambua ili mistari myeupe ionekane katika fito hizo.

38 Kisha akaweka fito alizozibambua kwenye mabirika yote ya kunyweshea mifugo, ili ziwe mbele ya makundi walipokuja kunywa maji. Wanyama walipokuja kunywa maji, hali wakiwa wanahitaji mbegu,

39 wakapandwa hizo fito zikiwa mbele yao, wanyama waliopata mimba mbele ya hizo fito, walizaa wanyama wenye mistari, madoadoa na mabakabaka.

40 Yakobo akawatenga wadogo wa kundi peke yao, lakini akazielekeza nyuso za hao waliobaki kwenye wale wenye mistari na weusi waliokuwa mali ya Labani. Hivyo akatenga makundi yake mwenyewe na wala hakuwachanganya na wanyama wa Labani.

41 Kila mara wanyama wenye nguvu walipohitaji mbegu, Yakobo aliweka zile fito kwenye mabirika mbele ya hao wanyama, ili wapandwe karibu na hizo fito,

42 lakini ikiwa wanyama walikuwa wadhaifu hakuziweka hizo fito. Hivyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wanyama wenye nguvu wakawa wa Yakobo.

43 Kwa njia hii Yakobo akastawi sana, tena akawa na makundi makubwa, watumishi wa kike na wa kiume na ngamia na punda.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/30-a582da6d02c6ee2fa5cb91f4c76a4ae2.mp3?version_id=1627—

Mwanzo 31

Yakobo Akimbia Kutoka Kwa Labani

1 Yakobo akawasikia wana wa Labani wakisema, “Yakobo amechukua kila kitu kilichokuwa cha baba yetu naye amepata utajiri huu wote kutokana na vile vilivyokuwa mali ya baba yetu.”

2 Yakobo akatambua kwamba moyo wa Labani kwake haukuwa kama ulivyokuwa mwanzo.

3 NdipoBwanaakamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na kwa watu wako, nami nitakuwa pamoja nawe.”

4 Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje machungani yalikokuwa makundi yake.

5 Akawaambia, “Naona moyo wa baba yenu kwangu sivyo kama ulivyokuwa mwanzoni, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami.

6 Mnajua kwamba nimemtumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote,

7 hata hivyo baba yenu amenidanganya kwa kubadilisha ujira wangu mara kumi. Hata hivyo, Mungu hakumruhusu kunidhuru.

8 Kama alisema, ‘Wenye madoadoa watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye madoadoa, kama alisema, ‘Wenye mistari watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye mistari.

9 Hivyo Mungu amechukua mifugo ya baba yenu na amenipa mimi.

10 “Wakati fulani majira ya kuzaliana niliota ndoto ambayo niliinua macho na kuona kwamba wale mabeberu waliokuwa wakipanda kundi walikuwa wa mistari, madoadoa na mabakabaka.

11 Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, ‘Yakobo.’ Nikamjibu, ‘Mimi hapa.’

12 Akasema, ‘Inua macho yako uone wale mabeberu wote wanaopanda kundi wana mistari, madoadoa au mabakabaka, kwa maana nimeona yale yote ambayo Labani amekuwa akikutendea.

13 Mimi ndiye Mungu wa Betheli, ulikomiminia ile nguzo mafuta na pale mahali uliponiwekea nadhiri. Sasa ondoka katika nchi hii mara moja urudi katika nchi uliyozaliwa.’ ”

14 Ndipo Raheli na Lea wakajibu, “Je bado tu tunalo fungu lo lote katika urithi wa nyumba ya baba yetu?

15 Je, yeye hatuhesabu sisi kama wageni? Sio kwamba ametuuza tu, bali ametumia hata na vile vilivyolipwa kwa ajili yetu.

16 Hakika utajiri wote ambao Mungu ameuchukua kutoka kwa baba yetu ni mali yetu na watoto wetu. Hivyo fanya lo lote lile Mungu alilokuambia.”

17 Ndipo Yakobo akawapandisha watoto wake na wake zake juu ya ngamia,

18 naye akawaswaga wanyama wote mbele yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa amechuma huko Padan-Aramu kwenda kwa baba yake Isaki katika nchi ya Kanaani.

19 Labani alipokuwa amekwenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumba ya baba yake.

20 Zaidi ya hayo, Yakobo alimdanganya Labani Mwaramu kwa kutokumwambia kwamba anakimbia.

21 Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto Eufrati akaelekea nchi ya vilima katika Gileadi.

Labani Amfuatilia Yakobo

22 Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia.

23 Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima katika Gileadi.

24 Ndipo Mungu akamjia Labani Mwaramu katika ndoto usiku na kumwambia, “Jihadhari usiseme neno lo lote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.”

25 Yakobo alikuwa amepiga hema lake katika nchi ya vilima katika Gileadi wakati Labani alipomkuta, Labani na jamaa yake wakapiga kambi huko pia.

26 Ndipo Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini? Umenidanganya na umewachukua binti zangu kama mateka katika vita.

27 Kwa nini ulikimbia kwa siri na kunidanganya? Kwa nini hukuniambia ili nikuage kwa furaha na nyimbo za matari na vinubi?

28 Hata hukuniruhusu niwabusu wajukuu zangu na kuwaaga binti zangu. Umefanya kitu cha kipumbavu.

29 Nina uwezo wa kukudhuru, lakini usiku uliopita Mungu wa baba yako alisema nami, akaniambia, ‘Jihadhari, usiseme neno lo lote kwa Yakobo liwe zuri au baya.’

30 Sasa umeondoka kwa sababu umetamani kurudi nyumbani kwa baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?”

31 Yakobo akamjibu Labani, “Niliogopa, kwa sababu nilifikiri ungeweza kuninyang’anya binti zako kwa nguvu.

32 Lakini kama ukimkuta ye yote aliye na miungu yako, hataishi. Mbele ya jamaa yetu, angalia mwenyewe uone kama kuna cho chote chako hapa nilicho nacho, kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba hiyo miungu.

33 Kwa hiyo Labani akaingia ndani ya hema la Yakobo na ndani ya hema la Lea na ndani ya hema la watumishi wawili wa kike, lakini hakukuta cho chote. Baadaye alipotoka katika hema la Lea, akaingia hema la Raheli.

34 Basi Raheli ndiye aliyekuwa amechukua ile miungu ya nyumbani kwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata cho chote.

35 Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani kwake.

36 Yakobo akakasirika na kumshutumu Labani, akisema, “Uhalifu wangu ni nini?” Akamwuliza Labani, “Ni dhambi gani niliyofanya hata unaniwinda?

37 Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu sisi wawili.

38 “Mpaka sasa nimekuwa pamoja nawe miaka ishirini. Kondoo wako na mbuzi wako hawajaharibu mimba, wala sijala kondoo waume kutoka katika makundi yako.

39 Sikukuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, nilibeba hasara mimi mwenyewe. Tena ulinidai malipo kwa cho chote kilichoibwa mchana au usiku.

40 Hii ndiyo iliyokuwa hali yangu: Niliumia kwa joto la mchana na baridi usiku, pia usingizi ulinipa a.

41 Ilikuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi.

42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaki, hakuwa pamoja nami, hakika ungenifukuza mikono mitupu. Lakini Mungu ameona taabu yangu na kazi ngumu ya mikono yangu, naye usiku uliopita amekukemea.”

43 Labani akamjibu Yakobo, “Wanawake hawa ni binti zangu, watoto hawa ni watoto wangu na makundi haya ni makundi yangu. Vyote unavyoviona ni vyangu. Lakini hata hivyo ninaweza kufanya nini kuhusu hawa binti zangu, au kuhusu watoto waliowazaa?

44 Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.”

45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe akalisimamisha kama nguzo.

46 Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo.

47 Labani akaliita Yegar-Sahaduthana Yakobo akaliita Galeedi.

48 Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi.

49 Pia liliitwa Mispa, kwa sababu alisema, “Bwanana aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.

50 Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.”

51 Pia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi.

52 Lundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru.

53 Mungu wa Abrahamu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.”

Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaki.

54 Yakobo akatoa dhabihu juu ya kilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko.

55 Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake, binti zake na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/GEN/31-e0fe49ce3caea1d72b29c266f40622fe.mp3?version_id=1627—