1 Mambo ya Nyakati 20

Kutekwa Kwa Raba

1 Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme hutoka kwenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni akaenda Raba na kuuzunguka huo mji kwa Jeshi, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akaushambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.

2 Daudi akachukua taji kutoka kwenye kichwa cha mfalme wao, uzito wake ulikuwa talanta mojaya dhahabu na ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua kiasi kikubwa cha nyara kutoka katika mji huo

3 na akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

Vita Na Wafilisti

4 Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamwua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai, nao Wafilisti wakashindwa.

5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji.

6 Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuweko na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.

7 Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamwua.

8 Hawa walikuwa ndio wazao wa Mrefai huko Gathi, nao walianguka kwa mkono wa Daudi na watu wake.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/1CH/20-1c460257f920ebb5a7dbb84ca3174e9b.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

one × three =