2 Samweli 24

Daudi Ahesabu Wapiganaji

1 Hasira yaBwanaikawaka tena dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi dhidi yao, akisema, “Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.”

2 Kwa hiyo mfalme akamwambia Yoabu, pamoja na majemadari wengi wa jeshi aliokuwa nao, “Nendeni kwa makabila yote ya Israeli kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na mwandikishe watu wapiganaji, ili niweze kujua idadi yao.”

3 Lakini Yaobu akamjibu mfalme, “BwanaMungu wako na azidishe vikosi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”

4 Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yaobu pamoja na majemadari wa jeshi, kwa hiyo wakaondoka mbele ya mfalme kuandikisha wapiganaji wa Israeli.

5 Baada ya kuvuka Yordani, walipiga kambi karibu na Aroeri, kusini ya mji ulioko kwenye bonde jembamba, ndipo wakipitia Gadi, wakaenda hadi Yazeri.

6 Walikwenda mpaka Gileadi pia eneo la Tahtimu-Hodshi, wakaendelea mpaka Dani-Yaani na kuzunguka kuelekea Sidoni.

7 Kisha wakaenda kuelekea ngome ya Tiro pamoja na miji yote ya Wahivi na ya Wakanaani. Mwishoni, walikwenda mpaka Beer-Sheba katika Negebu ya Yuda.

8 Baada ya kupita katika nchi nzima, walirudi Yerusalemu baada ya miezi tisa na siku ishirini.

9 Yoabu akatoa hesabu ya wapiganaji kwa mfalme: Katika Israeli kulikuweko watu 800,000 wenye uwezo wa kupigana na katika Yuda watu 500,000.

10 Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambiaBwana, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. EeBwana, sasa nakuomba, uondolee mbali hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

11 Kabla Daudi hajaamka kesho yake asubuhi, neno laBwanalilikuwa limemjia Gadi nabii, aliyekuwa mwonaji wa Daudi, kusema:

12 “Nenda mwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

13 Basi Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je, ije njaa ya miaka mitatu katika nchi yako? Au miezi mitatu ya kukimbia adui zako wakikufuatia? Au siku tatu za tauni katika nchi yako? Basi sasa, fikiri juu ya hilo na uamue jinsi nitakavyomjibu huyo aliyenituma.”

14 Daudi akamjibu Gadi, “Nitataabika sana. Afadhali tuangukie mikononi mwaBwana, kwa maana rehema zake ni kubwa, lakini usiniache nianguke mikononi mwa wanadamu.”

15 BasiBwanaakaruhusu tauni katika Israeli kuanzia asubuhi mpaka mwisho wa muda ulioamuriwa, wakafa watu 70,000 kuanzia Dani hadi Beer-Sheba.

16 Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu,Bwanaalihuzunika kwa sababu ya maafa akamwambia malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi.

17 Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambiaBwana, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kufanya kosa. Hawa ni kama kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”

Daudi Ajenga Madhabahu

18 Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi na kumwambia, “Panda ukamjengeeBwanamadhabahu kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi.”

19 Kwa hiyo Daudi akapanda kama vileBwanaalivyokuwa ameamuru kwa kinywa cha Gadi.

20 Arauna alipotazama na kuona mfalme na watu wake wanakuja kumwelekea, alitoka nje na kusujudu mbele ya mfalme kifudifudi, uso wake mpaka ardhini.

21 Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?”

Daudi akajibu, “Kununua sakafu yako ya kupuria, ili niweze kumjengeaBwanamadhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”

22 Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue cho chote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ng’ombe kwa ajili ya kuni.

23 Ee mfalme, Arauna anatoa vyote hivi kwa mfalme.” Pia Arauna akamwambia mfalme, “BwanaMungu wako na akukubali.”

24 Lakini mfalme akamjibu Arauna, “La hasha, nasisitiza kuvilipia. Sitatoa sadaka ya kuteketezwa kwaBwanaMungu wangu isiyonigharimu cho chote.”

# Kwa hiyo Daudi akanunua ile sakafu ya kupuria nafaka na maksai, akalipa shekeli hamsini za fedha.

25 Daudi akamjengeaBwanamadhabahu huko, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. KishaBwanaakajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.

—https://d1b84921e69nmq.cloudfront.net/337/32k/2SA/24-5ca31c9044d4e6473c118c288a2e9c90.mp3?version_id=1627—

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve + 19 =